Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyejifungua pacha watatu aomba msaada

Aliyejifungua pacha watatu aomba msaada

Muktasari:

  • Monica Maleo (37) mkazi wa kijiji cha Mbahe aliyejifungua pacha watatu ameiomba Serikali na watu wa kada mbalimbali kumsaidia kwa kuwa hana uwezo wa kuwalea watoto hao kutokana na ugumu wa maisha.

Moshi. Monica Maleo (37) mkazi wa kijiji cha Mbahe aliyejifungua pacha watatu ameiomba Serikali na watu wa kada mbalimbali kumsaidia kwa kuwa hana uwezo wa kuwalea watoto hao kutokana na ugumu wa maisha.

Kijiji hicho kipo kata ya Marangu Magharibi Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Monica ambaye ana watoto wengine watatu alijifungua pacha hao juzi Jumatatu Februari 22, 2021 katika hospitali ya Kilema iliyopo Marangu.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Februari 24, 2021 amesema hana shughuli ya kumuingizia kipato na mumewe kwa sasa hana kazi.