Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyesababisha kijana afungwe miaka 60 aiangukia mahakama

New Content Item (1)
Aliyesababisha kijana afungwe miaka 60 aiangukia mahakama

Muktasari:

  • Binti anayedai kumsingizia kijana mwenzake kumpa ujauzito na kusababisha kufungwa miaka 60 jela  afunguka mazito asema huenda wazazi wake walimshuku kutokana na kwamba walikuwa wakisoma wote shule moja.

Moshi. Maria Sanga(20)mkazi wa Kijiji cha kilingi wilayani Siha  anayedai kumsingizia Mwanafunzi  mwenzake kumbaka na  kumpa ujauzito nakupelekea  kufungwa miaka 60 jela amesema huenda wazazi wake walimshuku kijana huyo,Tumain Mfinanga kutokana na kwamba walikuwa walisoma wote shule moja.
Ameyesema hayo leo Februari Mosi wakati akizungumza na Waandishi wa habari Mjini Moshi ambapo amesema tukio hilo limekuwa likimuumiza katika maisha yake na kushindwa kuvumilia hali ambayo amesema anaoimba serikali imsaidie kumwachia kijana huyo kutokana na kwamba sio yeye aliyempa ujauzito.
Amesema alifanya hivyo kutokana na shinikizo kutoka kwa wazazi wake ambapo  walimlazimisha kwa kumtishia kumpiga ndipo alipomtaja kijana huyo ambaye anasema hahusiki na ujauzito wake.
Mwaka 2018 kijana huyo alikuhumiwa na mahakama ya wilaya ya Siha kutumikia kifungo cha miaka 60 jela kwa kosa la kumpa ujauzito binti huyo ambaye wakati huo  alikuwa kidato cha pili,mwaka 2017.
Pia amewashauri wasichana wenzake kuwa jasiri na kusema ukweli kwenye jambo ambalo halina ukweli ili kuweza kunusuru maisha ya wengine ambao hawana hatia na kuwasababishia majeraha ambayo hayaponi.
“Nawashauri wasichana wenzangu kukitokea jambo kama hili uwe na ujasiri wa kuweza kuongea na kuwa na ufafanuzi wa kusema ukweli haijalishi umri wako ni mdogo au ni mkubwa ,cha msingi ni kusema ukweli ili kila mtu awe huru na maisha yake.”