Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anayedaiwa kumuua mkewe kwa kunyimwa unyumba akamatwa

Anayedaiwa kumuua mkewe kwa kunyimwa unyumba akamatwa

Muktasari:

  •  Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kennedy Malekea (21), mkazi wa kijiji cha Msinga wilayani Rombo kwatuhuma za kumuua mkewe Fausta Silayo (22) kwa kumchoma visu vya tumboni na mgongoni kwa madai ya kunyimwa unyumba.


Moshi. Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kennedy Malekea (21), mkazi wa kijiji cha Msinga wilayani Rombo kwatuhuma za kumuua mkewe Fausta Silayo (22) kwa kumchoma visu vya tumboni na mgongoni kwa madai ya kunyimwa unyumba.

Marehemu Fausta alikuwa na mtoto mchanga wa mwezi mmoja alichomwa visu hivyo Julai 23 na kusababisha kifo chake Julai 24 alipokuwa akipelekwa hospitali ya Huruma kwa ajili ya matibabu.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa Kennedy huyo baada ya kutoweka kwa siku 25 na kukimbilia nchi jirani ya Kenya baada ya kutenda tukio hilo.

"Ni kweli amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea," amesema Kamanda Maigwa. 

Marehemu Fausta alizikwa katika kijiji cha Msinga wilayani Rombo kwa wazazi wake, Julai 31 mwaka huu ambapo ameacha watoto wawili mmoja ana umri wa mwezi mmoja na mwingine wa mwaka mmoja.