Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Auawa, mwili watelekezwa

Muktasari:

Mkazi wa Kijiji cha Mrere wilayani hapa, Venance Aloyce (29), ameuawa na mwili kutelekezwa eneo la Korongo Kitovata.

Rombo. Mkazi wa Kijiji cha Mrere wilayani hapa, Venance Aloyce (29), ameuawa na mwili kutelekezwa eneo la Korongo Kitovata.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona alisema jana kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha kifo.

“Mwili wa marehemu unafanyiwa uchunguzi kujua chanzo cha kifo hicho,” alisema Kamanda Makona.

Akisimulia tukio hilo mama mzazi wa kijana huyo, Mariselina Aloyce alisema mwanaye aliondoka nyumbani Desemba 27 na hakurudi.

Alisema msamaria mwema ambaye alipita eneo mwili huo ulipotelekezwa alimpa taarifa kuwa kuna mwili wa mwanaye umetelekezwa.

“Desemba 27 nilitoka nyumbani kwenda kanisani, niliwaacha wakiwa wamelala, baada ya kurudi kanisani nilienda kwenye sherehe maeneo jirani na hapa nyumbani,” alisema mama mzazi huyo.

“Niliporudi sikumkuta, jioni ilibidi niende kwenye kibanda kumuulizia kama alionekana maeneo hayo, niliporudi nyumbani kuna mtu akaja nyumbani akanambia kuna mtoto wenu amekufa na mwili wake umetelekezwa.”

Diwani wa Katangara Mrere, Venence Mallel alisema tukio hilo limetokea kwenye kata yake na kifo cha kijana huyo kina utata.

“Mwili wa kijana huyu umekutwa eneo la Kitovata, kwa mujibu wa wananchi mwili wake umefanyiwa ukatili wa aina mbalimbali,” alisema.