Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba akamatwa akitaka kumuozesha bintiye

Baba akamatwa akitaka kumuozesha bintiye

Muktasari:

  • Mkazi wa kijiji cha Emuguri,kata ya Njoro Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro(jina lake linahifadhiwa) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa madai ya kutaka kumuozesha binti yake wa miaka 11 kwa mahari ya ng'ombe watatu.

  

Same. Mkazi wa kijiji cha Emuguri,kata ya Njoro Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro(jina lake linahifadhiwa) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa madai ya kutaka kumuozesha binti yake wa miaka 11 kwa mahari ya ng'ombe watatu.

Tukio hilo lilitokea Agosti 7, mwaka huu katika kijiji hicho ambapo baba huyo aliandaa sherehe ya kimila  ya kumuaga binti huyo aliyekuwa aozeshwe na kijana wa Kata jirani ya Ruvu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa mzee huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

Kamanda Maigwa amesema wanamshikilia mzee huyo mwenye umri wa miaka 68 kwa uchunguzi wa tukio hilo na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

"Tunamshikilia mzee mmoja ambaye jina lake tunalihifadhi baada ya kumfanyia sherehe ya kimila binti yake kwaajili ya kumepeleka kwa mwanaume huko Ruvu ,bahati nzuri tulipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ndipo tulipomkamata,"amesema Kamanda Maigwa



Kutokana na tukio hilo, Kamanda Maigwa ametoa onyo kwa watu wenye tabia kama hizo za kuwaozesha watoto wadogo akisema hatua kali za kisheria  zitachukuliwa dhidi ya mzee huyo ili iwe fundisho kwa wengine  wenye tabia kama hizo.

Mwananchi digital ilipoitafuta familia ya binti huyo kujua ni kwanini binti huyo hakupelekwa shule na kutaka kuozeshwa walikataa kutoa ushirikiano na kusema hawawezi kuzungumza chochote kwa sasa.