Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bei vocha za simu za kukwangua zapanda


Muktasari:

  • Bei ya vocha za simu za kukwangua zimepanda kutoka Sh1,000 hadi Sh1,200 na iliyokuwa ikiuzwa Sh500 hadi Sh600.

Dodoma. Bei ya vocha za simu za kukwangua zimepanda nchini kutoka Sh1,000 hadi Sh1,200 huku Serikali ikiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha watoa huduma hawapandishi bei kiholela.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Mei 29, 2024, Mbunge wa Viti Maalumu, Tunza Malapo amehoji ni nini kauli ya Serikali kuhusu kupanda kwa bei ya vocha za kukwangua kwa kuwa zimepanda kutoka Sh1,000 hadi Sh1200.

“Vocha iliyokuwa inauzwa Sh500 sasa ni Sh600. Nataka kauli ya Serikali kwa sababu wananchi hawaelewi,”amehoji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Maryprisca Mahundi amesema jambo hilo limejitokeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo Tunduma, Mbozi na Songwe.

“Waheshimiwa wabunge wamekuwa wakilifuatilia na sisi tumefuatilia na kuagiza TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania), wahakikishe  watoa huduma hawapandishi bei kiholela lazima wafuate utaratibu,”amesema.

Katika swali la msingi, Malapo amehoji ni lini tatizo la mawasiliano ya simu kwa baadhi ya kata za jimbo la Mtwara mjini litaisha.

Akijibu swali hilo MaryPrisca amesema Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa ujumla wake inashughulikia upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijiji na baadhi ya maeneo ya mjini yaliyopo pembezoni yasiyo na mvuto wa kibiashara.

“Hivyo UCSAF itakwenda kufanya tathimini kwa maeneo ya Mtwara Mjini yaliyopo pembezoni na yasiyo na mvuto wa kibiashara kuona kata zipi zenye changamoto ya mawasiliano,  ili ziweze kuweka katika mpango wa kufikishwa mawasiliano katika mwaka wa fedha 2024/25.