Beyonce apata nafasi tisa tuzo za Grammy

Wednesday November 25 2020
tuzo beyonce pic
By Mwandishi Wetu


Majina ya wasanii wanaowania Tuzo ya Grammy Awards 2020 yametangazwa, ambapo mwanamuziki wa Marekani, Beyonce Knowles ameongoza kutajwa kwenye vipendele vingi.
Star huyo wa muziki Marekani atachuana na wakali wengine watatu ambao nao wametajwa kwenye vipengele vingi.
Beyonce ameibuka kwenye ‘nomination’ tisa akichuana na wakali Taylor Swift, Dua Lipa na Roddy Ricch.
Tuzo hizo ambazo ni za awamu ya 63 zitatolewa mjini Los Angeles nchini Marekani Januari 30, 2020
Beyonce ametajwa kwenye tuzo tisa katika vipengele nane ambapo wimbo wake wa ‘Black Parade’ alioutoa hivi karibuni umetajwa katika vipengele viwili.
Wimbo huo wa ‘Black Parade’ alioutoa kipindi cha kupinga mateso kwa Waafrika Weusi ‘Black Lives Matter’ umeingia katika kipengere cha Rekodi na Wimbo wa mwaka.
Taylor Swift pamoja na Dua Lipa ambao watampa ushindani Beyonce nao wametajwa kwenye vipengere sita.

Advertisement