Biteko asitisha uchimbaji, wananchi walimdanganya Rais

Muktasari:

  • Waziri Biteko asitisha shughuli za uchimbaji madini Chunya, baada ya wananchi kukiri kumdanganya hayati John Magufuli kumtuhumu mwekezaji.

Mbeya. Waziri wa Madini, Doto Biteko amepiga marufuku shughuli za uchimbaji wa madini katika Mlima Kaputa kata ya Chalangwa wilayani Chunya mkoani Mbeya  baada ya kubaini wananchi kuidanganya Serikali na kuwepo na chuki  binafsi na mwekezaji Joseph Mwazyele  kwa  kumdanganya Rais  hayati John Magufuli kuwa anachimba eneo la mradi wa  matenki ya maji na  makaburi na kupekea kuwepo kwa  mgogoro wa muda mrefu.

Biteko amesema  amefikia hatua hiyo na kukazimika kufanya ziara ya kujirisha na kubaini  mwekezaji alikuwa akimilki kihalali na kwamba mwekezaji huyo ajaliendele tangu alipofutiwa leseni mwaka 2019.

"Kwanza mmechuma dhambi mlimdanganya Rais kuwa mwekezaji huyo anachimba madini kwenye maeneo ya miradi na makaburi leo nimefika kuangalia uhalisia katika mlima huo na kubaini kuna udanganyifu kwani eneo hilo limevamiwa na wachimbaji wadogo kuanzia leo marufuku," alisema.

Biteko amesema kwa marufuku shughuli za uchimbaji kuendelea wakati  Serikali ikiangalia nini cha kufanya na mpaka utaratibu utakapowekwa na Wizara kupata taarifa na Serikali imejipanga.

Alisema kuwa pia Wizara imebaini kuwepo kwa utoaji leseni kiholela mchimbaji mmoja kumiliki leseni lukuki na kutokana na changamoto hizo Serikali imefuta leseni 7,000 ambazo zitatolewa kwa wachimbaji wadogo wa madino nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Saimon Mayeka Saimon alisema kuwa changamoto ya mgogoro huo umechangiwa pia na viongozi wa chama na wananchi wamekuwa wakilishwa maneno kwa migongo ya watu wengine.

"Sasa waziri kaagiza eneo hilo lisihusishwe tena na uchimbaji wa madini nitaweka ulinzi wa kutosha vijana watakaothubutu kuingia na kuchimba wakibainika watawajibishwa nasi tumejipanga kwani wananchi wa kata hii mnasifika kwa ukorofi,"alisema.


Mayeka alisema kuwa mgogoro huo kama Serikali waliufuatilia na kubaini mwekezaji huyo anamiliki kihalali na suala na kuchimba kwenya miradi ya maji na makaburi sio kweli bali ni mambo ya kiasa kuingizwa.

Mbunge wa Jimbo la Chunya, Masache Kasaka amewataka wananchi kuwa wavumilivu  na kusubiri maamuzi ya  Wizara ya Madini na kwamba wakubaliane na matokeo kutokana na mgogoro huo kudumu na kukwamisha maendeleo.

Kasaka alisema kuwa ujio huo wa waziri na kujiridhisha na kufanya maamuzi kwa kipindi hiki utaleta tija ya kuchochea shughuli  maendeleo katika kata ya Chalangwa kupitia madini ya  dhahabu inayopatikana katika mlima huo.