Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bulaya kugharamia wanafunzi wasio na uwezo


Muktasari:

  • Akizindua programu hiyo, jana Jumamosi Januari 3,2026 Bulaya amesema mpango huo utawahusu watoto wote wanaotoka kata 13 za Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara.    

Dar es Salaam. Mbunge wa Bunda Mjini (CCM), Ester Bulaya amezindua programu maalumu ya kuwasaidia watoto ambao wazazi hawana uwezo ili kutimiza ndoto zao kuendelea na elimu ya sekondari.

Bulaya amefafanua kuwa watoto hao ni wale ambao wamefaulu kwenda kidato cha kwanza, lakini wazazi wao hawana uwezo kuwagharamia mahitaji muhimu ya shule, ikiwamo sare, begi na viatu.

Akizindua programu hiyo, jana Jumamosi Januari 3, 2026 Bulaya amesema mpango huo utawahusu watoto wote wanaotoka kata 13 za Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara.

“Hadi ninazungumza wameshafika watoto zaidi ya 250, nimeshatumia zaidi ya milioni 40 kuwasaidia. Mpango huu endelevu unaitwa Bulaya Community Education Program,” amesema Bulaya.

Katika uzinduzi huo, Bulaya aliwakabidhi madaftari, viatu, mabegi na vifaa vya michezo vya shule.

“Jimbo la Bunda wapo wenye uhitaji katika kata zote, mwanzo nilisema nitaanza na watoto 100, lakini mahitaji yakaongezeka, siku na namna kama mbunge au kama mama. Mimi nimepitia hizi changamoto, nilipokuwa mdogo, lakini nikapata msaada hadi hapa nilipo,” ameeleza Bulaya.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi zake, alizoahidi wananchi wa Bunda kuwa ataendelea kuwashika mkono na kuwa na bega kwa bega katika changamoto zinazowakabili. 

Desemba 23, 2025 siku mbili kabla ya Sikukuu ya Krismasi Bulaya alitoa msaada wa vyakula katika taasisi mbalimbali zikiwamo za watoto wanaoishi katika mazingira magumu na gereza la Bunda.

Mmoja wa wasimamzi wa kituo la kulea watoto wanaoshi katika mazingira magumu kilichopo katika jimbo hilo, Mtawa Art Lleshaji amemshukuru Bulaya kwa moyo wake wa kujitolea, kujali ustawi wa jamii na kuendelea kuwa karibu na wananchi wake.