Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM yabariki uwekezaji wa bandari, yatoa maagizo serikalini

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao cha Hamashauri Kuu ya chama hicho ambacho kimejadili masuala mbalimbali ikiwemo mkataba wa uwekezaji na uendelezaji wa bandari baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai.

Dodoma. Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai wakibariki mchakato huo.

Katika kikao chake kilichoketi makao makuu ya CCM, jijini Dodoma leo Jumapili Julai 9, 2023 chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kikao hicho kimesema uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.

Taarifa fupi iliyosomwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema mbele ya waandishi wa habari ilesema uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, Ibara ya 59, ukurasa wa 92.

Hata hivyo, Mjema amesema kikao kimekubaliana kuwa, Serikali iendelee kutoa elimu kwa kwa wananchi katika jambo hilo.

"Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari," amesema Mjema.

Halmashauri hiyo ilifanyika baada ya kutanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ambapo pia imezipongeza Serikali zote mbili za Chama Cha Mapinduzi, Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.

Katika mkutano huo na waandishi, Mjema amesema siyo siku ya kujibu maswali kwani yeye amesoma kile ambacho wamekubaliana na Halmashauri na mambo mengine yasubiri wakati wake.