Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chalamila awatahadharisha waliopanga maandamano kupinga mkataba wa bandari

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amekitahadharisha kikundi cha watu wanaopanga kufanya maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji bandari kati ya Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amekitahadharisha kikundi cha watu wanaopanga kufanya maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji bandari kati ya Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai.

Pia amekemea upotoshwaji unaofanywa na watu wanaosema nchi imeuzwa na kwamba hata siku moja Rais (Samia Suluhu Hassan) hawezi kuuza nchi kwa kuwa ameapa kulinda nchi na kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Tahadhari hiyo imeitoa leo Juni, 19, 2023 wakati akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake, ikiwa ni muda mfupi baada ya Jeshi la Polisi kudhibiti maandamano yaliyopangwa kufanyika kwenda Ikulu kushinikiza kupinga mkataba huo.

Akiwa ofisini kwake Ilala Bomba, kiongozi huyo amesema maandamano yanachelewesha uchumi, husimamisha biashara, hufifisha utoaji huduma za afya pia kuleta taharuki.

“Nina uhakika watu hao hawajui wanachokifanya, pia hawajapitishwa vizuri kufahamu mkataba wa uendelezaji na ubia wa bandari vilevile hawajui tija wa makubaliano ya uendelezaji wa bandari. Hivyo Serikali iko tayari wakati wowote kueleza tija ya maendelezo na ubia wa bandari,”amesema.

Chalamila amesema maandamano siku zote hayana faida yoyote zaidi ni kuchelewesha uchumi, kusimamisha biashara, kufifisha huduma za afya na kuleta taaruki kwa jamii ambazo zitarudisha nyuma maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo RC Chalamila amewataka vijana au kikundi cha watu wanaopanga kufanya maandamano kutumia muda huo kupitia mkataba wa maendelezo na ubia wa bandari ili kujua nia njema ya Serikali na tija ya maendelezo hayo.