Changogo mwenyekiti mpya CCM Handeni

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Jumla ya kura zilizopigwa ni 1,578 ambapo kura halali ni 1554 huku 24 zikiharibika.

Handeni. Mgombea nafasi ya Mwenyekiti CCM wilaya ya Handeni, Amiri Changogo ametangazwa mshindi na kufanya chama hicho kupata kiongozi mpya baada ya yule wa awali jina lake kukatwa.

 Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu Oktoba 3, 2022 msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Leopold Abeid amesema Changogo amepata kura 1083 akifuatiwa na Ramadhani Diliwa kura 386 huku Ahamad Chihumpu akipata kura 85.

Pia msimamizi huyo amemtangaza Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe kuwa mshindi nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu taifa kwa kwa kupata kura 720, akifuatiwa na Charles Sungura 676 na Abeid Mkombati kura 627.

Hata hivyo Sungura ambaye pia aligombea nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu mkoa, ilibidi kutangaza kuachia nafasi hiyo kutokana na kushinda nafasi ya mkutano mkuu taifa.

Mwenyekiti aliyeshinda, Changogo amesema atakwenda kuiunganisha Serikali na chama katika wilaya hiyo ili kuhakikisha shughuli za usimamizi wa kazi za maendeleo zinafanyika.

"Nitasimamia shughuli zote za Chama Cha Mapinduzi, lakini nitakwenda kuwaunganisha Serikali yetu na chama nitafanya hayo kwa uwezo wa mwenyezi mungu nawashukuru sana nipo tayari saa yoyote kuwatumikia", amesema Changogo.

Jumla ya wajumbe wote waliotakiwa kuhudhuria katika mkutano huo ni 1739 na waliopiga kura ni wajumbe 1493 kutoka kwenye kata 33 za Handeni mjini na Vijijini.