Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chato wapata kivuko kipya

Muktasari:

Kivuko hicho ni miongoni mwa vivuko vinne vilivyogharimu zaidi ya sh 15 billion kujengwa nchini. 

Chato. Adha ya ukosefu wa kivuko iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa wilaya ya Chato na Geita imemalizika baada ya Wizara ya ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano kupitia wakala wa ufundi na umeme (Temesa) kupokea kivuko kipya cha Chato-Nkome kilichogharimu kiasi cha Sh 3.1 bilioni.
Kivuko hicho kilichokabidhiwa leo Januari 5, kimejengwa na kampuni ya Ukandarasi ya wazawa ya Songoro Marine ya jijini Mwanza na kina uwezo wa kubeba tani 100 za mizigo pamoja na abiria 200.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano Dk Leornad Chamuriho alisema kukamilika kwa kivuko hicho kutawezesha wananchi wa Chato,Nkome na maeneo mengine ya visiwani  kusafirisha bidhaa zao.
Awali mtendaji mkuu wa Temesa, Japhet Maselle akizungumza wakati wa mapokezi ya kivuko kipya cha Chato -Nkome alisema kivuko hicho ni miongoni mwa vivuko vingine vitatu vilivyojengwa na serikali katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwarahisishia wananchi usafiri


Ametaja vivuko vingine vilivyojengwa kuwa ni pamoja kivuko cha Nyamisati-Mafia, kivuko kipya cha Bugolora -Ukara pamoja na kivuko cha Kayenze-Bezi
Mbunge wa jimbo la Chato Dk Merdad Kalemani amesema kukamilika kwa kivuko hicho kutawezesha wafanyabiashara wa samaki na dagaa kupeleka bidhaa zao kwenye soko la kimataifa la samaki lililopo Kasenda sanjari na kuwarahisishia usafiri wafanyabiashara wanaosafirisha dagaa kwenda nje ya nchi.