Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chongolo asisitiza utatuzi kero za wananchi

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel  Chongolo akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa (DC), Shaka Hamdu Shaka leo Jumamosi mara baada ya kuwasilia Mkoa wa Morogoro kwa ziara ya kichama ya siku tisa. Picha na Bakari Kiango

Muktasari:

  • Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amenza ziara ya siku tisa mkoani Morogoro kwa ajili kusikiliza kero za wananchi, huku akisisitiza uboreshwaji wa sekta za afya, elimu, kilimo na miundombinu.

Morogoro. Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameanza ziara ya siku tisa mkoani Morogoro, itakayojikita kusikiliza kero za wananchi, huku akisisitiza utatuzi wa kero za wananchi katika sekta za afya, elimu, kilimo, miundombinu na vyanzo vya maji.

Ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yanayotarajia kufikia kilele chake Februari 5, 2023.

"Tumekuja kuangalia njia za kutafuta suluhisho ya changamoto zinazowakabili wananchi na si vingeinevyo. Tupo na wenzangu, tupo timamu kwa kutimiza wajibu huu," amesema Chongolo.

Chongolo ameanza ziara leo Jumamosi Januari 28, 2023 katika wilaya ya Gairo, akiambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema na Katibu wa Idara ya  Organaizesheni Issa  Haji Ussi (Gavu).

Akizungumza na wanachama wa CCM waliompokea mpakani mwa mkoa wa Dodoma na Morogoro, Chongolo amesema zira yake itaangalia suala la miundombinu ya barabara hasa wakati huu wa mvua zinazoendelea kunyesha kwa nyakati tofauti.

"Pale wananchi wanapokwama na viongozi tukwame ili tuwe na wajibu wa kurekebisha, tumekuja kuangalia masuala ya kilimo hasa upatikanaji wa pembejeo.

"Tunataka kujifunza na kujua changamoto tutakazozibeba kwa sababu ndio dhamana tuliopewa. Pia tutaangalia vyanzo vya maji ili kuhakikisha tunaondoa changamoto za upatikanaji wa maji inapatikana," amesema Chongolo.

Kwa upande wake, Mjema amesema "Tumekuja kuhakikisha tunakwenda kuiteteea na kuijenga CCM na kupata wananchama wengi zaidi kuliko mwaka jana.

“Tunakwenda kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao kwa kuhakikisha tunazipunguza," amesema Mjema.