Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CRDB yaendelea kufungua milango kwa Watanzania kuwekeza kwenye hisa

Muktasari:

 Mkutano mkuu wa 22 wa Benki hiyo unaendelea jijini Arusha, leo (Ijumaa) na kesho.

Arusha.  Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuwekeza kwenye hisa kutokana na kila kipato walichonacho.

"Tunaona ongezeko la kampuni kusajiliwa Soko la Hisa. Kutokana tulichonacho, kiwepo kwa ajili ya kula na mambo mengine lakini tusisahau kuwekeza kwa ajili ya baadaye. Hisa ni moja ya sehemu za kipato cha uhakika muda wowote," amesema Dk Kimei.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Ally Hussein Laay amesema mazingira yamebadilika hivyo wananchi wawekeze kwenye hisa.

"Zamani yeyote aliyemiliki hisa alikuwa anaonekana ni bepari tofauti na ilivyo sasa. Ukiwa na kipato cha kutosha wekeza Soko la Hisa Dar es Salaam, Nairobi au Kampala," amesema Laay.

Mwenyekiti huyo mpya wa bodi amechukua nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake, Martin Mmari ambaye muda wake umekwisha.