Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC aingilia kati kunyanyaswa kwa mjane

Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara, Janeth Mayanja akikwangua njia mpya kwa jembe ili kumwezesha kupita mjane Rose Bayo wa Kijiji cha Endaswold anayenyanyaswa na shemeji na wakwe ikiwemo kunyimwa sehemu ya kupita. Picha na Joseph Lyimo

Muktasari:

  • Mgogoro ulianza baada ya mjane kugoma kurithiwa na shemeji yake baada ya mumewe kufariki mwaka 2016.

Hanang'. Mkuu wa Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara, Janeth Mayanja amewaagiza wakwe na mashemeji wa Kijiji cha Endaswold kuacha mara moja kumnyanyasa na kumfanyia vitendo vya kikatili mjane Rose Bayo.

Janeth ametoa agizo hilo akiwa na wajumbe wa kamati ya usalama na watumishi wa idara ya ardhi alipotembelea kiwanja namba 1106  Block A kilichopo Endaswold kinachomilikiwa na mjane huyo ambaye mume wake alifariki mwaka 2016.

Baada ya kufariki kwa mume wake Joseph Bayo, mashemeji walitaka wamrithi na baada ya kukataa ndipo migogoro ilianza ikiwemo kumnyanyasa mjane huyo.

Mkuu huyo wa wilaya amemuagiza mkuu wa polisi wa wilaya hiyo (OCD) kuhakikisha askari polisi wanamchukulia hatua shemeji wa mjane huyo, Emmanuel Shauri anayechochea mgogoro na kumfanyia ukatili wa kijinsia.

Amesema eneo hilo ni eneo la makazi na limerasmishwa kwa kuwa na mchoro wa mipangomiji na upimaji ila wakwe zake waliziba njia iliyotumika tangu mwaka 2013 kwa kujenga nyumba mwaka jana  na kutengeneza kabuli la bandia kwenye njia inayomsaidia mjane huyo kupita.

Janeth ameihamisha barabara inayopita kwenye eneo la wakwe wa mjane huyo na kuwaagiza wananchi kupasua barabara ya mita tatu.

Mkuu wa Wilaya amewaagiza watalaamu kufanya marekebisho ya upimaji wa eneo hilo ili barabara iliyochongwa na wananchi irasmishwe.

"Ninawaagiza wakwe kuacha mara moja vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa mjane na vyombo vya dola vifuatilie usalama wake," amesema Janeth.

Kwa upande wake, Rose Bayo amemshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kutatua mgogoro huo na kumsaidia kupata sehemu ya kupita kwani  hakuwa na njia kwa kipindi kirefu baada ya wakwe zake kujenga nyumba kwenye njia na kuweka kaburi bandia.

"Waliweka kaburi lisilo na mwili na kujenga nyumba kwenye barabara tunayotumia na kusababisha sisi tushindwe kupita njiani ila sasa tunaweza kupita," amesema mjane huyo.