DC Ludewa amshukuru Rais Samia kwa fedha za zahanati ya kijiji

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva akiwa amepiga magoti akitoa shukrani kwa Rais Samia wakati wakimbiza Mwenge walipowasili wilayani hapo kukagua miradi ya maendeleo leo Jumanne, Aprili 25, 2023.

Muktasari:

  • Ujenzi wa zahanati hiyo ulianza mwaka 2022 kwa nguvu za wananchi kwa kufyatua matofali na michango mingine, ndipo baadae Serikali ikaunga mkono kwa kutoa fedha kukamilisha ujenzi huo.

Ludewa. Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva amepiga magoti kumshukuru Rais kwa fedha zilizotolewa kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kimelembe.

Amefanya hivyo leo April 25, 2023 wakati wamewasili na Mwenge wa uhuru kukagua zahanati hiyo ambayo ilianza ujenzi na nguvu za wananchi na baadae serikali kuunga mkono.

Amesema kukamilika kwa zahanati hiyo kutawasaidia wananchi wa eneo hilo kufuata huduma za afya mbali na eneo hilo.

“Ujenzi wa zahanati hii kuna saidia kutatua changamoto za kiafya ambazo zilikuwa zinapatikana kwa mda mrefu na mbali na eneo hili,” amesema Mwanziva.

Kwa upande wake Essau Haule mtendaji wa Kijiji cha Kimelembe amesema ujenzi wa zahanati hiyo ulianza mwaka 2022 kwa nguvu za wananchi na baadae serikali kuunga mkono kwa kukamilosha ujenzi huo.

“Ujenzi wa zahanati hii ulianza mwaka 2022 kwa nguvu za wananchi kwa kufyatua tofali na michango mingine ndipo baadae Serikali ikaunga mkono kwa kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huu,” amesema Haule.

Naye Jojina Mbawala mkazi wa kijiji cha Kimelembe amesema awali huduma za kiafya walikuwa wanaifuata kijiji jirani ambacho kinapatikana umbali wa kilometa mbili.