Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Sabaya aagiza aliyeuza eneo kwa wananchi asakwe

DC Sabaya aagiza aliyeuza eneo kwa wananchi asakwe

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameliagiza Jeshi la polisi kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani humo  kumsaka aliyekuwa mtendaji wa mtaa wa Jiweni kata ya Muungano, Sabore Mollel na kumkamata.

Hai. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameliagiza Jeshi la polisi kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani humo  kumsaka aliyekuwa mtendaji wa mtaa wa Jiweni kata ya Muungano, Sabore Mollel na kumkamata.

Mtendaji huyo anatuhumiwa kuingilia eneo la serikali lenye ukubwa wa ekari 22.5 na kuliuza kwa wananchi, kinyume cha taratibu.

Sabaya ametoa agizo hilo leo Alhamisi Februari 25, 2021 mara baada ya kutembelea eneo hilo na kusikiliza wananchi waliodai kuuziwa na kupiga marufuku wananchi kusogelea eneo hilo ambalo.

Amesema mwaka 1984 eneo hilo lilibainishwa kama eneo la mji wa Hai na mwaka 1988 likaingizwa kwenye mpango na kutengua hati zote za kimila.

"Ndugu wananchi naomba mtambue kuwa mwaka 1984, eneo hili liliingizwa kwenye mpango miji na mwaka 1988 likaingizwa kwenye mpango kabambe, mwaka 1993 wakati mnadai mligawiwa na uongozi wa serikali ya kijiji, waligawa eneo ambalo halikuwa kwenye mamlaka yao, lilikuwa tayari ni mali ya umma chini ya Halmashauri.”

"Sasa naliagiza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Takukuru, mhakikishe mnamkamata Mollel huyu alifukuzwa kazi tangu 2017 lakini bado anafanya kazi za kitapeli kama mtumishi na ana muhuri wa kijiji hiki,” amesema.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Yohana Sintoo amesema eneo hilo ni mali ya Serikali na lilipangwa kama eneo la dampo.