Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Slaa: Serikali irekebishe kasoro mkataba DP World

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Balozi Willibrod Slaa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkataba wa Bandari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Sunday George

Dar es Salaam. Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Sweden, Dk Willibrod Slaa ameishauri Serikali irekebishe kasoro zinazolalamikiwa kwenye mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hoja hiyo ya Dk Slaa inapigilia msumari kauli iliyoibuliwa na viongozi wa dini juzi, walioitaka Serikali kwenda kwa wananchi kuwafafanulia vifungu vyote vilivyoibua mijadala ili kuwatoa hofu na kurekebisha kasoro zitakazobainika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dk Slaa alisema: “Naomba ieleweke bila chembe ya wasiwasi wowote kuwa, taarifa hii haina dhamira yoyote ya kupinga uwekezaji wa kweli na wenye tija kwa manufaa ya Taifa letu.”

Alieleza shaka inayoibuka kutoka kwa wananchi kuwa yanatokana na rejea ya mikataba mbalimbali ambayo Serikali iliwahi kuingia na mataifa mengine na ikaleta changamoto.

Aliitaja mikataba hiyo ni pamoja na ule wa Serikali na Symbion Power Tanzania Limited, Richmond, IPTL na mingine.

Dk Slaa alisema usiri uliogubika mchakato wa mkataba huo, ni miongoni mwa kasoro zinazotajwa, hivyo alisisitiza hakukuwa na sababu ya wananchi kupata taarifa baada ya kuvuja. “Kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alionekana akishuhudia uwekaji saini wa mkataba, ni busara ya kawaida Taifa kuarifiwa juu ya mikataba hiyo,” alisema.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Sheria za Kimataifa, Wakili Peter Madeleka alisema Serikali inapaswa kutoa elimu kwa wananchi, badala ya kumuita mkosoaji mmojammoja.

“Endapo kila mmoja atapata ukweli wa jambo hili hakuna atakayeitwa mpotoshaji, shaka iliyopo imetokana na masuala ya kisheria,” alisema.
Hata hivyo, azimio la mkataba huo tayari limesharidhiwa na Bunge, lakini kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe alisema kuna haja ya kuona kampuni itakayoundwa baada ya kuingiwa kwa mkataba umiliki wake unakuwa wa 50 kwa 50.

Alisema kati ya DP World na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ni lazima kuwe na usawa.

Alisema kilichopitishwa na Bunge ni azimio la ushirikiano baina ya nchi mbili, lisipotekelezwa kwa miezi 12 linakufa.

Kwa mujibu wa Zitto, kwa kuwa asilimia 67 ya mauzo ya nje ya Dubai na jiografia yao, ni muhimu kushirikiana nao, lakini ili kujenga uwezo wa ndani na baada ya kuwa na uwezo itakuwa rahisi kuwanunua kwa asilimia 100.

“Nimetazama takwimu na tija ya bandari yetu tunaweza kufuta kodi zote nchini tukabakiza ushuru wa forodha tu bandarini na nchi ikaenda bila shaka,” alisema.

Kuhusu Zitto alisema; “Bandari ni jambo la Muungano, lakini kama ilivyo mafuta na gesi utekelezaji wake sio wa muungano. Zanzibar wana shirika lao la bandari. Kwa Mujibu wa Sheria yetu ya bandari, hata Mtwara inaweza kuwa na kampuni yake ya kujiendesha.”

Kauli ya LHRC

Katika hatua nyingine, katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga aliitaka Serikali irejee upya vipengele vya mkataba vyenye changamoto ya kisheria, vilivyoibua mijadala na kiwango cha umiliki wa sehemu ya uwekezaji kiwekwe wazi, ili wananchi waelewe faida itakayopatikana.