Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Idadi ya wauguzi, wakunga yafikia 47,000

Msajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Nchini, Agnes Mtawa (wa katikati) akizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma juu ya mafunzo yanayotolewa na baraza hilo kwa wakunga na Wauguzi Nchini. Picha na Beldina Nyakeke

Muktasari:

Idadi ya wauguzi na wakunga wenye leseni imeongezeka kutoka asilimia 80 mwaka 2019 nakufikia asilimia 95 mwaka huu.

Musoma. Idadi ya wauguzi na wakunga nchini imefikia 47,000 huku matumizi ya dijitali yakitajwa kuchangia asilimia 95 kati yao kuwa na leseni kwa mwaka 2023 kutoka asilimia 80 mwaka 2019.

Takwimu hizo zimetolewa mjini Musoma leo Oktoba 13, 2023 na Msajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Nchini,  Agnes Mtawa wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadili, sheria na taratibu za kazi kwa wauguzi na wakunga.

"Kabla ya mfumo wa kidijitali wauguzi na wakunga walikuwa wakiuhisha leseni zao kwa njia ya kawaida ambapo wengine walikuwa wakilazimika kutuma fomu kwa njia ya basi hivyo fomu zingine zikawa zinapotelea njiani kabla hazijafika hali iliyokuwa ikipelekea baadhi yao kushindwa kupata leseni zao kwa wakati," amesema

Kutokana na urahisi kwa sasa amewataka wauguzi na wakunga kuhakikisha kila mmoja ana kuwa na leseni kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.

Kuhusu maadili, kanuni na sheria, msajili huyo amesema malalamiko dhidi ya utendaji kazi wa wauguzi yamepungua ingawa hakuweza kutoa takwimu kwa maelezo kuwa hali hiyo inatokana na elimu ya mara kwa mara ambayo wamekuwa wakitoa kwa wauguzi na wakunga nchini.

"Mfano kwasasa tupo hapa Mara tunakutana na wauguzi na wakunga kwenye halmashauri zote kuwakumbusha  umuhimu wa  kufanyakazi kwa kuzingatia maadili, kanuni na sheria za kazi," amesema

Ameongeza lengo la baraza  hilo kufanya ziara na kutoa elimu  kwenye kila mkoa ni kutaka wauguzi na wakunga kutoa huduma bora na za staha kwa wagonjwa bila kuleta manung'uniko.

"Tunafanya mafunzo haya mara kwa mara lengo nikutaka kuzuia na sio kusubiri hadi malalamiko yatokee, mfano kwa mkoa wa Mara huu mwaka hatujapokea malalamiko yoyote,"amesema

Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mara, Stanley Kajuna amesema mafunzo ya baraza hilo yanasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa.

"Kuna changamoto ya upungufu wa wauguzi na wakunga kwenye mkoa wetu... kuna wauguzi na wakunga 1,347 sawa na asilimia 35 kati ya wauguzi zaidi ya 3,000 wanaohitajika," amesema

Ameongeza kutokana na upungufu huo wanalazimika kufanya kazi kwa zaidi ya saa 12 badala ya saa 8 kwa mujibu wa utaratibu huku wakilazimika kupumzika mara moja kwa wiki badala ya mara mbili.

"Pamoja na changamoto hizo bado tunafanyakazi kwa kuzingatia sheria, maadili na taratibu za kazi na hii imetokana na mafunzo ya mara kwa mara yanayotolewa na baraza," amesema