Infinix Note 12 VIP kuvunja rekodi chaji 100% dakika 17 tu

Muktasari:

  • Teknolojia, leo tutaizungumzia simu mpya aina ya Infinix NOTE 12 VIP ambayo imekuwa gumzo baada ya kuzinduliwa huko Ugaibuni, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kama GSMArena vimeeleza kuwa kampuni ya simu za mkononi Infinix imevunja kizuizi cha kuchaji na kuitambulisha Infinix NOTE 12 VIP yenye kupokea chaji ya watt 120.

Teknolojia, leo tutaizungumzia simu mpya aina ya Infinix NOTE 12 VIP ambayo imekuwa gumzo baada ya kuzinduliwa huko Ugaibuni, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kama GSMArena vimeeleza kuwa kampuni ya simu za mkononi Infinix imevunja kizuizi cha kuchaji na kuitambulisha Infinix NOTE 12 VIP yenye kupokea chaji ya watt 120.

Watt 120 ya Infinix NOTE 12 VIP hutumia dakika 17 tu kwa simu yenye asilimia 0 kujaa kwa 100% kutokana na usitadi wa pampu ya chaji mbili na ikiwa huwezi kusubiri kwa dakika hizo dakika 10 zinatosha kuipa simu chaji asilimia za kutosha kutumia kwa siku nzima kufanyia kazi za kiofisi huku ukiendelea kubaki mitandaoni pasipo simu kuishiwa chaji.

Infinix NOTE 12 VIP inatumia MediaTek Helio G96 ambayo ina alama bora za Antutu 9 ni sawa na kusema Infinix NOTE 12 VIP inauwezo mkubwa wa uendeshaji Ram ya ukubwa wowote na kufanya mfumo mzima wa uendeshaji features nyengine katika simu kuwa rahisi kama ambavyo ilivyo kwa scrini ya NOTE 12 VIP yenye refresh rate 120HZ kuleta majibu ya haraka pale tu unapogusa kioo na hii kupelekea wapenzi wa games za mitandaoni kufurahia Zaidi.

Mali G57 MC2 ni mojawapo ya GPU zenye nguvu katika simu za bei ya kati, ambayo hufanya Infinix NOTE 12 VIP kuwa na nguvu Zaidi kuliko simu yoyote mahiri za bei hiyo ya kati.

Kulingana na sifa hizi chache ambazo zimeonekana kuongelewa na Blog hiyo huku kwa nchi kama Tanzania ambayo simu hii bado kufika inabaki kuwa hadithi, je simu hii itakuja Tanzania? Na je sifa za simu hii zitabaki kuwa hizi au itakuwa na mabadiliko? na je simu hii endapo ikitua Tanzania itapatikana kwa bei gani? Majibu ya haya maswali utayapata @infinixmobiletz