Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jambazi sugu lanaswa Dar

Muktasari:

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro alidai jana kuwa mtuhumiwa huyo, mkazi wa Goba alihusika kwenye matukio ya ujambazi katika maeneo mbalimbali akitumia gari hilo.

Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imemkamata mtuhumiwa sugu wa ujambazi akiwa na bastola aina Browning, magazine mbili, risasi 11 na gari aina ya Noah.

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro alidai jana kuwa mtuhumiwa huyo, mkazi wa Goba alihusika kwenye matukio ya ujambazi katika maeneo mbalimbali akitumia gari hilo.

Katika tukio jingine, Sirro alisema polisi wakiwa kwenye doria walikamata mfuko uliokuwa na risasi 20 za silaha aina ya G3.

Alisema tukio hilo lilitokea Jumamosi saa  sita mchana eneo la uwanja wa mpira wa Chamanzi Mbagala, baada ya  askari waliokuwa doria kuwatilia shaka watu watatu.