Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jiji la Dodoma lawatumia salamu waliotelekeza mapagale

Muktasari:

Halmashauri ya Jiji la Dodoma limesema litachukua hatua kwa kuzingatia sheria ya mipango miji kwa wamiliki wa mapagale yote ambayo yametelekezwa na kugeuka vichaka katika kata ya Kikuyu Kusini jijini hapa.

Dodoma. Halmashauri ya Jiji la Dodoma limesema litachukua hatua kwa kuzingatia sheria ya mipango miji kwa wamiliki wa mapagale yote ambayo yametelekezwa na kugeuka vichaka katika kata ya Kikuyu Kusini jijini hapa.

Akizungumza na wakazi wa kata hiyo mara baada ya zoezi la usafi leo Jumamosi Januari 29,2022, Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji hilo, Joseph Mafuru amesema Jumatatu (Januari 31) atatuma kikosi kazi kitakachobaini mapagale hayo ambayo yamegeuka maeneo ya kujifichia vibaka.

Amesema maofisa hao watakagua vibanda vyote ambavyo vimejengwa kiholela katika kata hiyo kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi kulingana na Sheria za Mipango Miji na Umilikishwaji wa Ardhi.

"Kuna eneo nimeliona, nilitaka kulifanyia kazi ila nikasema nisubiri nijiridhishe kwanza, ila kwa kuwa mmetoa malalamiko yenu hapa mbele ya viongozi wote. Nitayafanyia kazi na Jumatatu nitatuma kikosi kazi changu kushughulika na eneo hili,"amesema.

Aidha, amesema wapo katika mchakato wa kuhakikisha unawapatia viwanja jumla ya wananchi 328 wa Kata ya Kinyambwa wa Jijini humo ambao mashamba yao yalichukuliwa na Jiji kwa ajili ya uendelezaji wa Jiji hilo.

Amesema mpaka hivi sasa wameshatoa viwanja 25 kati ya 328 ambapo zoezi la upimaji linaendelea ili kuweza kukamilisha haraka na kugawa viwanja hivyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri ameagiza uongozi wa Kata hiyo kushirikiana na Kamati ya ulinzi na usalama kuhusu suala la usalama kutokana na kuibuka kwa vitendo vya wizi pamoja na mauaji katika eneo hilo.

"Naomba viongozi husika mjadili haya masuala ya usalama kama ajenda wapo wakristo wanaenda kwenye jumuiya kila Jumamosi au siku maalum waliyopanga hebu muongelee na masuala ya upendo mnapokutana haiwezekani watu wanafikia hatua yakutoana uhai suala hili halikubaliki,"amesema.