Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jinsi nzige wanavyomtesa waziri, naibu wake

Jinsi nzige wanavyomtesa waziri, naibu wake

Muktasari:

  • Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda na naibu wake, Hussein Bashe wamewasili wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro kusimamia shughuli ya kuwadhibiti nzige walioingia jana wilayani humo.

Siha. Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda na naibu wake, Hussein Bashe wamewasili wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro kusimamia shughuli ya kuwadhibiti nzige walioingia jana wilayani humo.

Nzige hao waliingia wilayani humo jana Jumanne Februari 24, 2021 wakidaiwa kutoka wilayani Longido na kuonekana maeneo mbalimbali, tayari ndege kwa ajili ya kuwadhibiti imeanza kufanya kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Februari 24, 2021 Profesa Mkenda amesema Serikali imejipanga kutumia nguvu kubwa kuwaangamiza nzige hao.

"Hili kundi la nzige walioingia hapa Siha inaonekana wametokea Longido kwa hiyo tulichokifanya asubuhi tumemwaga sumu kuwaangamiza nipo hapa na naibu waziri wangu kuhakikisha tunatumia nguvu kubwa kuwaangamiza.”

"Tutahakikisha nzige wote wanaangamia ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za kilimo kama kawaida, niwaondoe hofu wananchi wa Siha na Tanzania kwa ujumla hawa nzige baada ya siku mbili wote tutakuwa tumeshawaangamiza," amesema Profesa Mkenda