Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Joti azungumzia afya ya Vengu

Joti

Muktasari:

Pamoja na kulazwa Muhimbili, Vengu alipelekwa India na kuanzia wakati huo hajawahi kuonekana tena hadharani.

Dar es Salaam. Baada ya kuwepo kwa kimya kirefu kuhusu hali ya msanii, Joseph Shamba maarufu Vengu, msanii mwenzake Lucas Muhavile ‘Joti’ amezungumzia hali yake.

Vengu ni kati ya wasanii watano waliojizolea umaarufu kupitia kundi la The Original Comedy lililokuwa na wasanii akiwemo Joti, Mpoki, Masanja Mkandamizaji na Wakuvanga ambalo lilikuwa likirusha vichekesho vyake kituo cha EATV na baadaye kuhamia TBC.

Vengu ana miaka zaidi ya sita sasa tangu aanze kuumwa na taarifa zake zilianza kuzagaa Septemba 2011.

Pamoja na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, (MNH) alipelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi na kuanzia wakati huo hajawahi kuonekana tena hadharani.

Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 12, Joti amesema Vengu anaendelea vizuri japokuwa bado hajaweza kuamka kitandani.

Amesema kadri siku zinavyozidi kwenda afya yake inawapa matumaini na wana imani ipo siku atanyanyuka na kuendelea na shuguli zake huku akiwataka Watanzania kuendelea kumuombea.

Kuhusu tetesi za kwamba wamemtelekeza, Joti amesema suala hilo halina ukweli na kufafanua kwamba, labda watu walitaka wakiwa wanakwenda kumsalimia waite vyombo vya habari, jambo ambalo si sahihi kwani mgonjwa anahitaji faragha.

“Yule ni mwenzetu na hatuwezi kumuacha pamoja na matatizo aliyonayo sasa hivi na mara kwa mara tunaenda kumsalimia nyumbani kwake na sio kama watu wanavyosema kuwa hatumtembelei,” amesema.