Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kampuni kurejesha Sh27 bilioni Serikalini

Kampuni kurejesha Sh27 bilioni Serikalini

Muktasari:

  • Kampuni ya Badr East Africa Enterprises, iliyokuwa ikitekeleza mradi mkubwa wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe, imeridhia kurejeshe Sh27 bilioni ilizolipwa na Serikali baada ya kughushi nyaraka.

Moshi. Kampuni ya Badr East Africa Enterprises, iliyokuwa ikitekeleza mradi mkubwa wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe, imeridhia kurejeshe Sh27 bilioni ilizolipwa na Serikali baada ya kughushi nyaraka.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ametoa kauli hiyo jana Jumatatu Julai 12, wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro, ambapo amesema mradi huo umekuwa pasua kichwa na atahakikisha huduma bora ya maji safi na salama mkoani humo.

Aweso amesema mkandarasi huyo,  Badr East Africa Enterprises Ltd alighushi  nyaraka za uongo zilizosababisha kulipwa fedha hizo ambapo baada ya kushikiliwa na kuhojiwa na vyombo vya dola alikiri kughushi nyaraka hizo na kuahidi kurejesha fedha.

"Kwa sasa Sh27 bilioni zinarejeshwa, lakini si kurejeshwa tu, lazima tupate funzo, utekelezaji wa miradi ya maji unaanza na upatikanaji wa mkandarasi mzuri, ukimpata mkandarasi pasua kichwa, madhara yake ni makubwa sana"amesema Aweso

Ameongeza "Tumejifunza mengi sana kupitia mradi huu, niwaombe sasa wataalamu, vikao na michakato isiyo ya ulazima tuachane nayo, tushaweka mambo yetu sawa, sasa ni kazi tu na zege halilali"

Amesema kwa sasa wizara hiyo kupitia kwa wataalamu wake wa ndani wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wanaendelea na baadhi ya shughuli katika mradi huo ikiwemo ufungaji wa mabomba kutoka Kisangara-Kiverenge -Vudoi yenye urefu wa kilomita 70 ambapo mpaka sasa wamefunga kilomita 44.

Aweso amewataka wataalamu wa maji katika mradi huo kuacha tabia ya kuhujumu mradi huo ambapo alitolea mfano eneo la Kisangara lililoandikiwa ripoti ya kuhitajika kufungwa pampu za kuvutia maji 11 wakati uhalisia zinahitajika pampu 6 pekee.

Waziri huyo ameongeza kuwa, katika bajeti ya Serikali 2021/22 imetenga Sh19 bilioni kwa ajili ya kushughulikia matatizo ya maji mkoa wa Kilimanjaro.