Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigoma waomba kambi ya madaktari bingwa

Wananchi wa Wilaya ya Kasulu na maeneo ya jirani wakiwa katika foleni ya kujiandikisha kwa ajili ya kupata vipimo na matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo,  baada timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni, kuweka kambi ya siku tano wilayani humo.

Muktasari:

  • Wananchi wilayani Kasulu wameiomba serikali na taasisi binafsi kuweka utaratibu wa kuwasogezea karibu  huduma za kibingwa mara kwa mara ili waweze kupata matibabu na kupunguza gharama za kusafiri kuzifuata katika hospitali za rufaa.

Kasulu. Wakazi wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wameiomba Serikali na taasisi binafsi kuwa na utaratibu kwa kuwawekea kambi ya madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali angalau mara moja kwa mwezi.

Hilo litawawezesha kupata huduma za kitatibu na kupunguza gharama za kusafiri kuzifuata.

Wananchi hao walitoa rai hiyo leo Mei 25,2024 katika Hospitali ya wilaya ya Kasulu baada ya kupata matibabu kwa madaktari bingwa kutoka hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni, chini ya ufadhili wa Taasisi ya LALJI  Foundation na Hiltop iliyowezesha kambi ya siku tano.

Mkazi wa Kasulu mji, Juma Bujuibili  amesema wananchi wengi wanaishi maeneo ya vijijini na vipato vyao vya chini  hawamudu gharama za kufuata huduma za kibingwa katika hospitali za rufaa hivyo, wengi kujikuta wakiathirika na kupoteza maisha kwa kukosa matibabu ya kibingwa.

Naye Yona Kazamaso amesema, “Nimefika kupata matibabu baada ya kupata taarifa za uwepo wa kambi hii, nimefurahi kwani huwa inatulazimu kusafiri hadi  Bugando au Kigoma mjini kupata huduma za kibingwa.

Mwenyekiti wa LALJI Foundation,  Imtiaz Lalji amesema  wameamua kufadhili kambi hiyo ili kusaidia kuboresha afya za wana Kigoma.

“Tumefanya hivi kwa sababu  familia yetu  wote ni wazaliwa wa Mkoa wa Kigoma, hivyo tunahakikisha wanapata matibabu ya kibingwa ili kulinda afya zao,”amesema.

Daktari bingwa wa upasuaji, Dk Frank Sudai amesema wagonjwa wengi aliowapokea wamebainika kuwa na tatizo la shinikizo la juu la damu ambalo linatokana na mfumo wa maisha na ulaji usiozingatia lishe bora.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Semistatus Mashimba  amesema wananchi zaidi ya 1,800 kwa siku nne kati ya tano wamejitokeza kupata huduma hizo za kibingwa.

“Tutaenda kuliangalia jambo hilo kwa kushirikiana na wadau ili kuwe na utaratibu wa uwepo wa kambi kama hii ili kuwapunguzia mzigo wa gharama wananchi ambao wengi wao ni wa kipato cha chini wasioweza kufuata na kumudu gharama za huduma za kibingwa kwenye hospitali za rufaa,”amesema Mashimba.

“Tumekuwa tukizunguka mikoa mbalimbali nchini kutoa huduma hizi lakini tumeona Kigoma kuna uhitaji mkubwa wa huduma za kibingwa,                        tunaenda kujipanga ili kurudi kwa mara ya pili,”amesema Mkurugenzi wa Game Frontiers, Mohammed Taki.