Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kihenzile: Wataalamu logistiki zingatieni katiba kuepusha migogoro

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akizungumza kwenye uzinduzi wa Chama cha Lojistiki na Usafirishaji (Talta), uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Hivi sasa mchango wa sekta ya lojistiki na usafirishaji kwenye pato la taifa ni asilimia 6.5 hivyo baada ya miaka mitno wanataka kufikia asilimia 10.

Dar es Salaam. Serikali imewataka Chama cha Wataalam wa Lojistiki na Usafirishaji Tanzania (Talta) kuzingatia katiba yao ili kuepusha migogoro, migongano na kuhasimiana wenyewe.

Chama hicho kimetakiwa kushirikiana na vyama vingine vya kitaalamu huku wakikumbuka Wizara ndiyo msimamizi mkuu hivyo wanatikiwa kushirikiana nayo kila wakati.

Akizungumza leo Mei 9, 2025 Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile kwa niaba ya Waziri Makame Mbarawa katika uzinduzi wa chama hicho uliofanyika jijinj Dar es Salaam amesema ni mategemeo yao kitafanya mambo mbalimbali ikiwepo utafiti kwa ajili ya kusaidia wataalam wa ndani na nje ya chama.

Amesema wakifanya hayo itachangia na kusaidia uwekekezaji unaofanywa na sekta ya umma kuwa endelevu na chachu ya maendeleo ya Taifa.

"Tunaamini chama kitaandaa makongamano, semina na mafunzo pamoja na tafiti za uchapishaji kwa ajili ya kuongeza uelewa wa wataalamu hasa kwa taasisi ya umma na binafsi kwa wanaofanya shughuli za lojistiki na  usafirishaji "amesema Kihenzile.

Pia, amesema Serikali inaweza kufanya maamuzi sahihi kutokana na tafiti ndogo na kubwa zitakazokuwa zinafanywa kwa kushirikiana na vyombo vya kitaalamu.

Hata hivyo, Kihenzile ametoa rai kwa niaba ya Profesa Mbarawa kwa uongozi wa Talta kwa kujikita kwenye weledi na kuunganisha wataalamu kama ilivyo kwenye vyama vingine.

Vilevile amesema chama hicho kijaribu kukaa chini na kuja na majawabu ya mambo muhimu ya changamoto kuu pamoja na maboresho ya kujenga yale yanayotakiwa.

"Tuwaombeni pia msimamie kuhakikisha madereva katika sekta hii waliopo binafsi na umma wanapata maslahi yao na niwasihi wamiliki wa vyombo mbalimbali mnazingatia maslahi ya wafanyakazi,"amesema.

 Awali, rais wa Talta, Alphonce Mwingira amesema malengo ya chama hicho ni kwa ajili ya kusaidia sekta ya umma na binafsi ili kubaini namna bora ya kumiliki, kudhibiti na kusimamia namna ya kuendesha shughuli zinazohusiana na lojistiki na usafirishaji nchini.

"Hivi sasa mchango wa sekta yetu kwenye pato la taifa ni asilimia 6.5 na wakati tunajadiliana tulisema hapana kama sekta hii inafanya vizuri basi tutafika asilimia 10 na tunaamini kwa kuongeza weledi wa sisi wataalamu ndani ya miaka mitano tutafikia malengo," amesema Mwingira.

Naye, Halima Mbwana, ambaye alipata ajali wakati akiendesha basi la kampuni ya Super Feo, iliyosababisha kukatika mkono mmoja amesema tasnia ya madereva bado haijapata mtetezi.

"Naibu Waziri naomba uendelee kupigania tasnia hii kutafuta mtetezi ili kuondoa msongo wa mawazo ya madereva na kuepukana na ajali za barabarani,dereva ana kazi nguvu na kuputia magumu,"amesema na kuongeza kuwa

"Dereva atoke ofisini amekwazana na baosi wake, aje barabarani akutane na trafiki, kwenye basi akutane na biria wake na kwa Latra nanakutana na kidhibiti mwendo (VTS) na nyumbani ameacha mume au mke anakatuna nae kwenye malumbano."

Amesema linapotokea tatizo lifuatiliwe ili kujua limesababishwa na nini na hakika madereva wahukumiwe kwa haki zao na hili lifike mezani kwa ajili ya madereva kupewa heshima zao