Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kijana abuni mashine ya kumwagilia dawa shambani

Muktasari:

  • Mabilika amebuni mfumo wa umwagiliaji dawa  ili kuwarahisishia wakulima kukabiliana na wadudu waharibifu shambani

Dar es Salaam. Kijana Innocent Mabilika (25) amebuni mashine inayoweza kuwasaidia wakulima kupulizia dawa za kuua wadudu katika mashamba yao kwa urahisi na gharama nafuu.

Mabilika ambaye hajasomea ubunifu huo, amesema hayo leo Julai 2, 2025 alipozungumza na Mwananchi katika Maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ua Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yanayoendelea jijini hapa.

Kwa mujibu wake, mashine hiyo aliyobuni hutumia lita tano za mafuta kwa saa tano ambazo huweza kupulizia ekari 5 ksa siku.
“Niliamua kubuni hiki baada ya kuwa kati ya wale waliohangaika katika ukuaji wao, nilikuwa nikimsaidia mama kumwagilia nyanya chungu anazolima na tulikuwa tukitumia muda mrefu jambo lililofanya nijiulize nawezaje kupunguza kazi hii,” amesema.

Akiwa nyumbani kwao alianza kubuni mashine ya aina hiyo kwa kutumia plastiki za aina mbalimbali hadi kukamilika kwake ambapo baadaye alianza kufanya maboresho.

“Zile plastiki nilikuwa naunga kwa moto lakini nilichotengeneza kilikuwa na muonekano kama mashine kweli lakini ufanyajikazi wake haukuwa na ufanisi kama ulivyokusudiwa, baadaye nilishikwa mkono na Sido Mpanda lakini kwa sababu ya uchache wa vifaa wakanipeleka chuo cha Veta Mpanda,”amesema.

Pia, amesema alipofika Veta Mpanda walimuambia aoneshe mashine aliyokuwa ametengeneza ndipo aliwapa muonekano wa mashine ya kupukuchua mahindi na baada ya ukaguzi alisema inawezekana.

“Baada ya hapo nilianza kutengeneza mashine akisaidiwa kimawazo na utendaji hadi nilitengeneza mashine inayoonekana na yenye uwezo wa kufanya kazi ya chuma,” amesema.

Pia, amesema baada ya kumaliza hilo akiwa Veta, alianza kusimama mwenyewe ili aweze kuendelea kufanikisha ndoto zake ndipo aliingia mtaani na kuanza kuomba kuchomelea kwa mafundi waliopo kama masaidizi.

“Katika kuchomelea, kwa sababu ubunifu wangu sikutengeneza madirisha au milango bali  zana za kilimo, nilijaribu kujiendeleza mara nyingi zaidi. Ndiyo maana kila kidogo nilicholipwa nilikitunza ili niweze kukitumia kutengeneza mashine ninayohitaji,” amesema.

Baadaye kazi anazofanya kuonekana, watu wakaanza kuweka oda jambo lililoongeza uzoefu wake hadi kumfanya kuanza kuingia katika soko la mkulima kidogokidogo.

“Japokuwa si sana, naweza kupata oda leo nikakaa miezi mitatu hadi minne ndiyo napata oda nyingine. Lakini tangu Februari mwaka huu nimekuwa na uwezo wa kutengeneza mwenyewe. Nanunua injini ya pikipiki na mabati natengeneza hadi kukamilika,” amesema.

Amesema tangu mwaka 2020 alipoanza kufanya ubunifu huo hadi sasa lengo lake ni kumsaidia mkulima kufanya shughuli zake kwa urahisi na kupata tija ya kilimo aliyokuwa akiihitaji.

Mashine hiyo iliyoonekana kuvutia watu wengi hasa wakulima wanaolima bidhaa za mbogamboga na matunda, inagharimu Sh5 milioni.

“Unajua kwa sasa ni ngumu mtu kumudu mashine kubwa za kisasa zenye uwezo wa kufanya kazi kubwa kama ilivyo hii. Hii ni gharama nafuu na inarahisisha kazi. Ukitumia pampu ya mgongoni ni ngumu kumaliza hata ekari moja kwa saa moja, sasa ukiwa na hii ndani ya saa tano umefanya zaidi ya ekari tano ni rahisi,” amesema John Philipo mkazi wa Morogoro.