Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikwete akutana na Tume ya Haki Jinai

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akiwasili kwenye ukumbi wa kikao cha Tume ya Haki Jinai jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kutoa maoni yake katika tume hiyo.Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

  • Raia mstaafu amewasili tayari kutoa maoni kwa tume ya kuangalia mfumo wa haki jinai.

Dar es Salaam. Rais mstaafu, Jakaya Kikwete amewasili katika Ukumbi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) tayari kwa mahojiano na tume ya kuangalia mfumo wa haki jinai.

Kikwete amewasili ukumbini hapo saa 4:23 asubuhi na kupokewa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Mohammed Chande Othman na wajumbe wengine.

Kwa mujibu wa tume hiyo, Rais huyo mstaafu ndiye mjumbe wa mwisho kupokea maoni yake baada ya makundi mbalimbali kusikilizwa.

Baada ya kuwasili alifikishwa katika moja ya chumba kabla ya dakika tano baadaye kupelekwa katika ukumbi maalum wa kutoa maoni hayo.

Tume hiyo iliyoanza kazi Februari 6, mwaka huu imeshafanya mahojiano na makundi mbalimbali katika Mikoa 14 na Wilaya 30.

Baada ya Kikwete, kinachosubiriwa kwa hamu ni ripoti ya tume hiyo iliyopangiwa kufanya kazi kwa siku 120.

Kabla ya Kikwete wengine vigogo wengine mbalimbali walishatoa maoni yao, akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda.