Kiwanda chasimamisha uzalishaji, wakulima wa muhogo walia

Friday February 26 2021
lindipic

Lindi. Wakulima wa zao la muhogo wamesema wanapata hasara kutokana na Kiwanda  cha kusindika zao la muhogo, Casava Starch Tanzania Corporation (CSTC) kusimamisha uzalishaji kwa madai ya ukata wa fedha.  

Kiwanda hicho kilichopo Halmashauri ya Mtama, mkoani Lindi,kimesimamisha uzalishaji kwa miezi minane sasa na kusababisha watumishi 400 kukosa kazi huku ikidaiwa baadhi ya mitambo imeondolewa na kusafirishwa kusikojulikana.

Afisa Tawala wa kiwanda hicho, Knowless Lumambo, amekiri kusimamisha uzalishaji kwa madai ya kukosekana kwa fedha za uendeshaji.

Knowless Lumambo amesema kwa sasa wanatafuta fedha kutoka kwenye taasisi mbalimbali za kifedha ili kazi ya uzalishaji ianze mara moja.

Kuhusu hatima za watumishi 400 wanaodaiwa kuachishwa kazi, Lumambo hakuwa tayari kuzungumzia kwa madai liko juu ya mamlaka yake.

Baadhi ya wakulima wa Mtama, akiwemo mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mihogoni, Shabani Ally, Mwanaisha Yusufu, Abdallah Juma na Michael David kwa nyakati tofauti wamesema kutofanya kazi kwa kiwanda hicho kumewasababishia hasara kubwa

Advertisement

Walisema Zaidi ya tani 40 ziko katika nyumba zao na walidhani ujio wa kiwanda hicho ungekuwa mkombozi kwao.

Kiwanda hicho cha Casava Starch Tanzania Copration (CSTC) kilifunguliwa na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa, mwishoni mwa mwaka jana.

Imeandikwa na Mwanja ibadi

Advertisement