Kumbukumbu ajali ya MV Bukoba, ilivyoua mamia ya watu

Muktasari:

  • Mei 21, 1996, MV Bukoba ilizama katika ziwa Viktoria na kusababisha vifo vya watu Zaidi ya 800 huku baadhi ya watumishi wa Serikali wakishtakiwa kwa kosa la jinai kutokana na ajali hiyo.

Dar es Salaam. Ni miaka 27 imepita sasa tangu Tanzania ikumbwe na simanzi kubwa baada ya ajali ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba itokee Mei 21, 1996 iliyokuwa ikitoka Bukoba kuelekea Mwanza.

Ajali hiyo inayotajwa kusababishwa na kuzidisha mizigo na idadi ya watu katika meli iliua zaidi ya watu 800.

Baada ya kutokea kwa ajali hiyo, aliyekuwa Rais wa Tanzania kwa kipindi hicho, Benjamin Mkapa alitangaza siku tatu za maombolezo huku baadhi ya watumishi wa Serikali wakichukuliwa hatua kutokana na ajali hiyo.

Watumishi hao walioshitakiwa kwa makosa ya jinai; tisa walitokea Shirika la Reli Tanzania (TRC), Nahodha na Meneja wa TRC Divisheni ya Maji.

Meli hiyo ilizama baada ya kuzidiwa na uzito wa abiria pamoja na mizigo.