Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwimba yataja siri kushika namba moja mtihani wa ‘Mock’ Kanda ya Ziwa

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Ng'wilabuzu Ludigija akimkabidhi mwanafunzi zawadi baada ya wilaya hiyo kufanya vizuri kwenye mtihani wa Mock kwa kushika namba moja kati ya shule 4889 za halmashauri 43.

Muktasari:

  • Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza imekuwa ikisifika kwa mimba za utotoni, lakini sasa imejipatia sifa mpya baada ya kushika namba moja katika mtihani wa utimilifu wa darasa la saba Kanda ya Ziwa uliofanywa na shule 4,889 za halmashauri 43.

Mwanza. Halmashauri  ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza imeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza katika mtihani wa utimilifu wa darasa la saba (Mock) kwa mwaka 2025, ikitaja uwajibikaji kati ya walimu, wanafunzi na uongozi wa wilaya hiyo kuwa ni siri ya mafanikio hayo.

Akizungungumza leo June 3, 2025 wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi (motisha) kwa walimu na wanafunzi wa shule za msingi wilayani Kwimba baada ya kuwa wa kwanza Kanda ya Ziwa, Ofisa Elimu Taaluma- Msingi wilayani humo, Simburya Simburya amesema katika mtihani huo uliohusisha mikoa ya Mara, Simiyu, Shinyanga, Kagera, Geita na Mwanza wao wameibuka namba moja kwa Halmashauri zote 43 zenye shule 4,889.

Amesema wamekuwa wakwanza kwa vigezo vyote, kuanzia wastani hadi ufanisi na kuwa hata yale masomo waliyokuwa wakifanya vibaya kama vile hesabu, kiingereza na sayansi na teknolojia nayo wameongoza kwa kushika namba moja.

“Katika kigezo cha wastani tunasema katika ufanisi tuna alama 199.6 sawa na alama 200 kwahiyo tunaufaulu wa daraja A, lakini pia tumekuwa wakwanza kwa kigezo cha asilimia..kama matokeo haya yangekuwa yanawapeleka watahiniwa sekondari tungefaulisha kwa asilimia 97.86 huu ni ufaulu mzuri sana maana ni asilimbia mbili tu ndiyo imekosekana,”amesema.

Nakuongeza, “Hisabati tumekuwa wakwanza kwa ufaulu wa asilimia 96.64, Kiingereza wa kwanza kwa asilimia 95.73 pia na somo la Sayansi na Teknolojia tumekuwa wakwanza kwa ufaulu wa asilimia 93.87”

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dk Amon Mkoga amesema motisha, matumizi ya zana za kujifunzia pamoja na ushirikiano ya wanafunzi, walimu na maofisa imekuwa chahu kwao  kushika nafasi ya kwanza Kanda ya Ziwa.

Kutokana na ufaulu huo, amewaahidi walimu wa shule zilizofanya vizuri kwenda Zanzibar kufurahia ushindi huo huku akiwataka walimu kuendelea kufanya kazi nzuri ya kufundisha na endapo wana changamoto zozote wasisite kwenda kumueleza ili aangale namna ya kuzitatua.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Ng'wilabuzu Ludigija (kushoto) akimkabidhi herufi za kufundishia wanafunzi wa awali mmoja wa walimu wa wilaya hiyo.

 Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba,  Ng’wilabuzu Ludigija amewapongeza walimu pamoja na maofisa elimu kata na Wilaya kwa kuhakikisha wanabadilisha taswira ya Wilaya hiyo kwa kuwa na ufaulu mzuri huku akiwataka kufanya vizuri katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba unaotarajiwa kufanyika miezi ya hivi karibuni.

Huku, akiwataka maofisa elimu kuendelea kuandaa utaratibu wa kutoa motisha kwa shule na walimu wanaofanya vema ili kuwapa moyo wa kuendeleza juhudi katika kazi zao, Ludigija amewaambia walimu kuwa Serikali imeboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na itaendelea kuiboresha ili kila mtoto apate elimu bora.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amekabidhi zana za kufundishia na kujifunzia wanafunzi wa shule za awali wilayani humo ambazo zimetengenezwa na walimu waliopewa mafunzo ya ufundi stadi, zilizokabidhiwa kwa walimu wa kuu.

Mwalimu wa Shule ya Msingi Shiranona Kata ya Wala, Chausiku Magere anayetengeneza zana hizo zikiwemo vihesabio na karatasi zenye namba amesema chanzo cha kuendelea kuongeza ufaulu ni pamoja na kuandaa na kutumia zana hizo zinazosaidia kukabiliana na tatizo la kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu.

“Zana zinamsaidia mtoto kuwa na kumbukumbu na udadisi katika kile anachofundishwa hivyo kupunguza kazi kwa mwalimu. Lakini walimu tumejiwekea mikakati ya kutoa mazoezi ya kila wiki, mitihani ya ujilani mwema pamoja na mitihani ya wilaya inayofanyika kila mwezi,”amesema Chausiku.