Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LSF kutekeleza kampeni msaada wa sheria ya Mama Samia

Wajumbe wa Kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia wakiwa katika kikao kazi maalum kilichoketi kwenye Ofisi za LSF Dar es Salaam chini ya uratibu wa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na wadau wengine ili kupitia mkakati wa utekelezaji kampeni hiyo baada ya kuzinduliwa.

Muktasari:

  • Kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ilizinduliwa mnamo Februari 15, ambapo itaendeshwa kwa takribani miaka mitatu nchi nzima.

Dar es Salaam. Shirika la Legal Services Facility (LSF) limejipanga kutekeleza kampeni msaada wa kisheria ya Mama Samia iliyozinduliwa Februari 15, 2023 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro.

Ili kutekeleza kampeni hiyo, kikosi kazi kilichojumuisha wadau kutoka Serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali kimejadii maeneo makuu matatu ya kampeni hiyo.

Malengo hayo ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala ya utawala wa sheria pamoja na haki za binadamu, kujengea uwezo wadau katika mnyororo wa kutoa haki pamoja na kuboresha mifumo, sera na sheria ili kukuza upatikanaji wa haki nchini.

Akizungumzia kampeni hiyo baada ya kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni hiyo, Lulu Ng’wanakilala amesema jukumu la shirika hilo ni kuchochea upatikanaji  haki na kuleta nguvu ya pamoja kwa wadau wanaushughulikia masuala ya haki, usawa na sheria hapa nchini.

“Kwa takribani miaka 11 sasa tumekuwa tukitekeleza mradi wa upatikanaji wa haki kwa kuwezesha watoa huduma za msaada wa kisheria zaidi ya 4,000 na mashirika 184 Tanzania Bara na Zanzibar.

“Kuwepo kwa idadi kubwa ya wasaidizi wa kisheria na mashirika tunayoyapatia ruzuku kumewezesha huduma za msaada wa kisheria kutolewa kila mkoa na kila wilaya;

“Hii imesaidia kupungua kwa migogoro inayoenda mahakamani kwani asilimia 60 ya mashauri takribani 90,000 yanayoletwa kwa watoa huduma za kisheria kila mwaka hutatuliwa,” amesema Ng’wanakilala

Amesema kuwa wanawajengea uwezo kupitia uwezo kwa kuwapatia kozi za kisheria na haki na kuwajenga mifumo ya utawala bora, uendeshaji wa kiprogramu na usimamizi wa kifedha kwa mashirika yanayopokea ruzuku.

Akifafanua zaidi kuhusu jitihada zinazofanywa na LSF ili kutengeneza mfumo endelevu wa kitaasisi katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria nchini amesema;

“Matarajio yetu ya kuona kwamba wananchi wanajua haki zao, kunakuwa na mifumo thabiti na uboreshaji wa ushirikiano wa wadau kwa kuchochea juhudi za makusudi kuchukuliwa ili kuboresha sekta ya msaada wa kisheria nchini,” amsema na kuongeza;

“Tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali na wadau katika kuhakikisha tunawafikia watu wengi zaidi hususani maeneo ya pembezoni.” amesisitiza Ng’wanakilala.