Lukuvi afuta hati za vitalu viwili Mwanza

Muktasari:

  • Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefuta hati ya kutalu cha ardhi namba 153 na 154 kilichopo kata ya Mhandu jijini Mwanza.

Mwanza. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefuta hati ya kutalu cha ardhi namba 153 na 154 kilichopo kata ya Mhandu jijini Mwanza.

Ametoa maamuzi hayo leo Jumatano Machi 3, 2021 katika ziara ya siku nne mkoani humo ambapo ameamuru kufutwa kwa hati hizo ili maeneo hayo yamilikiwe na wananchi kisheria.

Kitalu namba 153 kimefutiwa hati yake baada ya mmiliki wake,  Abdallah Muhsen Malik kujiondoa katika umiliki wa eneo hilo.

Lukuvi afuta hati za vitalu viwili Mwanza

Pia,  Lukuvi ametoa siku 30 kwa kamishna wa ardhi jijini Mwanza kukamilisha taratibu za kisheria ili umiliki wa kitalu namba 154 ufutwe rasmi na kumilikishwa upya kwa wananchi wanaoishi katika eneo hilo.

Katika kitalu namba 154 kitamilikishwa kwa kaya 74 huku kaya 46 zikipatiwa umiliki wa kitalu namba 154.