Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabula ayazuia makampuni nane kupima ardhi

Mabula ayazuia makampuni nane kupima ardhi

Muktasari:

  • Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, Angelina Mabula ameyapiga marufuku makampuni nane yanayojihusisha na upimaji wa ardhi mkoa wa Kilimanjaro baada ya  kushindwa  kukamilisha upimaji wa ardhi ili kurasimisha maeneo ya wananchi kwa ajili ya kupatiwa hati.

Moshi. Naibu Waziri wa Ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ameyapiga marufuku makampuni nane yanayojihusisha na upimaji wa ardhi mkoa wa Kilimanjaro baada ya  kushindwa  kukamilisha upimaji wa ardhi ili kurasimisha maeneo ya wananchi kwa ajili ya kupatiwa  hati.

Amesema ni marufuku makampuni hayo kufanya kazi mkoani humo na kwamba serikali itaangalia makampuni mengine ambayo yamekuwa yakifanya kazi vizuri katika maeneo mengine.

Mabula ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Idara ya ardhi,wenye makampuni na wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi , sambamba na zoezi la kugawa hati miliki Mkoani humo.

Aidha amesema makampuni hayo yamekusanya zaidi ya Sh1.2 bilioni kutoka kwa wananchi na kwamba wameshindwa kukamilisha zoezi hilo kwa wakati ambapo pia ameagiza bodi kuhakikisha inachunguza makampuni hayo kama yalikuwa na sifa ya kufanya kazi hiyo.

"Naelekeza halmashauri zote mnapoingia mikataba na makampuni haya chunguzeni kama wana sifa ya kufanya kazi,tutaomba bodi ichunguze kama kweli mnao uwezo wa kufanya kazi, na tukibaini hamna huo uwezo tutawafutia usajili, haiwezekani makampuni yote nane mka `prove failure’ (mkashindwa ),” amesema Mabula.