Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madiwani wa CCM Pwani wapatiwa mafunzo maalumu ya uwajibikaji

Baadhi ya madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mafunzo yaliyofanyika leo Jumamosi, Juni 13, 2026, Wilayani Kibaha. Picha: Sanjito Msafiri

Muktasari:

  • Mafunzo hayo yanatarajiwa kuimarisha uwajibikaji na kasi ya utatuzi wa kero za wananchi katika maeneo yao.

Kibaha. Madiwani 185 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kata zote za Mkoa wa Pwani wamepatiwa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo kuhusu uajibikaji, uzalendo, na namna ya kuibua na kutatua kero za wananchi.

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Juni 13, 2026 Wilayani Kibaha ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wake, Mchengerwa amewataka madiwani kwenda kuyafanyia kazi maarifa waliyopata kwa kusimamia maendeleo ya wananchi na kuhakikisha kero zinazowakabili zinatatuliwa kwa wakati.

Aidha amesema baadhi ya viongozi wa vijiji wanapaswa kujirekebisha kwa namna wanavyosimamiarasilimali za wananchi, akibainisha kuwa si sahihi kuona fedha nyingi zikibaki kwenye akaunti za vijiji wakati wananchi wanaendelea kuteseka kutokana na kero ndogondogo zinazoweza kutatuliwa kwa kutumia fedha hizo.

“Unakuta kijiji kina fedha nyingi kwenye akaunti lakini wananchi wake wanaendelea kupata shida kwa sababu ya kero ambazo zingeweza kutatuliwa kwa urahisi.

“Hili halikubaliki, Madiwani mkiwa wenyeviti wa maendeleo katika kata mnawajibika kufuatilia matumizi sahihi ya rasilimali hizo kwa manufaa ya wananchi,” amesema.

Pia Mchengerwa amewataka madiwani kuwa mfano wa uadilifu, uwajibikaji na uzalendo katika maeneo yao, akisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea viongozi wanaosikiliza na kutatua changamoto zao kwa vitendo.

Baadhi ya madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mafunzo yaliyofanyika leo Jumamosi, Juni 13, 2026, Wilayani Kibaha. Picha: Sanjito Msafiri

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Kitete Mfilinge, ambaye ndio alikuwa mratibu, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea madiwani uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa weledi zaidi na kuongeza ufanisi katika kusimamia maendeleo ya wananchi.

Amesema mafunzo hayo yamejikita katika masuala ya uajibikaji, uzalendo, usalama wa nchi, utatuzi wa migogoro na kero za wananchi pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya viongozi wa chama na Serikali.

“Mkoa wa Pwani umeamua kuwa kinara wa mabadiliko kwa kuwajengea uwezo madiwani wake. Tunaamini maarifa haya yatawasaidia kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi na kusimamia maendeleo ya maeneo yao,” amesema Mfilinge.

Baadhi ya madiwani walioshiriki mafunzo hayo walieleza kuwa yatawasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Baadhi ya madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mafunzo yaliyofanyika leo Jumamosi, Juni 13, 2026, Wilayani Kibaha. Picha: Sanjito Msafiri

Diwani wa Kata ya Misugusugu, Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Ally Simba amesema mafunzo hayo yamewapa mwanga mpya kuhusu wajibu wao wa kusimamia maendeleo na kushughulikia changamoto za wananchi kwa wakati.

“Tumepata elimu muhimu itakayotusaidia kuwa karibu zaidi na wananchi wetu, kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka,” alisema Simba.

Naye Latifa Agustino, amesema mafunzo hayo yataongeza uwezo wa madiwani kusimamia miradi ya maendeleo na kuhakikisha rasilimali za wananchi zinatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa.

“Maarifa tuliyopata yatatusaidia kutekeleza wajibu wetu kwa ufanisi mkubwa zaidi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo wanayostahili,” amesema Agostino

Mafunzo hayo ni mara yake ya kwanza kufanyika kwa madiwani wote wa CCM Mkoa wa Pwani, hatua inayotarajiwa kuimarisha uwajibikaji na kasi ya utatuzi wa kero za wananchi katika maeneo yao.