Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maelfu wafurika Uwanja wa Jamhuri kumuaga Magufuli

Utaratibu kuaga mwili wa Magufuli wabadilishwa

Muktasari:

  • Idadi kubwa ya watu kutoka Dodoma, mikoa ya jirani na nje ya nchi wamefika katika Uwanja wa Jamhuri  jijini humo kuaga mwili wa Hayati Rais John Magufuli.


Dodoma. Idadi kubwa ya watu kutoka Dodoma, mikoa ya jirani na nje ya nchi wamefika katika Uwanja wa Jamhuri  jijini humo kuaga mwili wa Hayati Rais John Magufuli.

Wakazi hao walioanza kuingia uwanjani saa 12.00 asubuhi  wamesema walifika kuanzia saa 11 alfajiri kuwahi kuingia ndani ya uwanja.

Angel Josam ambaye amesafiri kutokea mkoani Singida akibainisha kuwa ameingia uwanjani hapo saa 11:03 alfajiri, “niliona nikichelewa kifika naweza kukosa nafasi ndani ya uwanja, nikaona niwahi, sikutaka kukaa nje ya uwanja, nataka nimuage mpendwa wetu ndani ya uwanja ndio maana nimewahi.”

"Nimetokea mkoani Singida kuja Dodoma ili kumuaga Rais Magufuli, licha ya kuwa nimeona na kusikia taarifa za kifo chake lakini nahisi kama bado tupo naye, sasa nimekuja nishuhudie mwenye.”

Mkazi mwingine Geofrey Sifuni amesema  amewasili uwanjani saa 12.34 akitokea wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Amesema kifo cha Magufuli ni pigo kwa Taifa na mtu mmoja mmoja.