Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama ya Kisutu yasimamisha usikilizwaji kesi ya Lissu

Muktasari:

  • Lissu anakabiliwa na kesi mbili za jinai katika Mahakama ya Kisutu, ikiwemo ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu  imesimamisha usikilizwaji wa kesi ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni, inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu kwa muda usiojulikana.

Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo kutokana na kuwepo kwa mashauri mawili ya maombi ya mapitio yaliyofunguliwa na Lissu Mahakama Kuu, akiiomba Mahakama hiyo ipitie na kufuta mwenendo wa Mahakama ya Kisutu wa Juni 16, 2025.

Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mhini anayesikiliza kesi hiyo, leo Jumanne, Julai Mosi, 2025 amesema kutokana na kuwepo kwa mashauri hayo ambayo yanahusu uamuzi wa mahakama yake, usikilizwaji wa kesi hiyo utasimama kusubiri uamuzi wa Mahakama Kuu katika mashauri hayo aliyoyafungua Lissu.

Hakimu Mhini amesema tarehe ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo itatolewa kwa njia ya wito rasmi wa Mahakama.

Katika mashitaka yote Lissu anadaiwa  kuchapisha taarifa za uongo katika mtandao wa Youtube, kinyume na Sheria ya Makosa ya Kimtandao namba 14 ya mwaka 2015, kifungu cha 16.

Katika mashitaka hayo, Lissu anadaiwa kumuhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutenguliwa kwa wagombea wa chama chake katika maeneo mbalimbali wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, 2024.

Pia anadaiwa kuwatuhumu askari Polisi kuhusika katika wizi wa kura kupitia vibegi, na majaji kutokutenda haki kwa madai ya kutaka wapate uteuzi wa Rais kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani.