Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yaamuru Tanzania kuilipa IPTL Sh426 bilioni

Muktasari:

Kutokana na mgogoro uliopo kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kampuni ya IPTL, mahakama ya migogoro ya kimataifa (ICSID) imeiamuru Serikali ya Tanzania kulipa Dola 185.4 milioni (zaidi ya Sh426 bilioni) kwa kukiuka mkataba

Dar es Salaam. kutokana na mgogoro uliopo kati ya Tanesco na kampuni ya IPTL, mahakama ya migogoro ya kimataifa (ICSID) imeiamuru Serikali ya Tanzania kulipa Dola 185.4 milioni (zaidi ya Sh426 bilioni) kwa kukiuka mkataba.

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) liliingia makubaliano ya kuzalisha umeme na IPTL (Independent Power Tanzania Limited) mwaka 1995 lakini mwaka 2013 kukawa na kutoelewana kati ya wahusika wa mkataba huo.

Katika makubaliano hayo, IPTL iliyokuwa inamilikiwa kwa ubia kati ya kampuni ya Mechmar ya Malaysia na VIP Engineering and Marketing ya Tanzania ilitakiwa kuzalisha megawati 100 kwenye mitambo yake iliyosimikwa Tegeta jijini Dar es Salaam na kuiuzia Tanesco.

Kutekeleza mkataba huo, IPTL ilikopa fedha kutoka kwa taasisi tofauti za fedha zikiwamo benki za nchini Malaysia kwa ahadi ya kurejesha kutokana na mapato itakayokuwa inayapata ikilipwa na Tanesco.

Baada ya muda, madeni yote iliyokuwa nayo IPTL yalinunuliwa na Benki ya Standard Chartered tawi la Hong Kong. Benki hununua deni kama mteja anataka kukopa tena na hupewa kiasi kinachobaki baada ya deni alilonalo kulipwa.

Ni katika makubaliano haya kati ya Standard Chartered na IPTL ndipo Tanesco ilipotakiwa kutoa dhamana ya mkopo huo na endapo itashindwa kuulipa basi Serikali ichukue jukumu hilo.

Kuhakikisha malipo hayo yanafanywa kwa wakati na mhusika anazipata, makubaliano hayo yaliafiki kufunguliwa kwa akaunti ya Escrow Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambako Tanesco ingekuwa inapeleka marejesho ya mkopo huo.

Baadaye, Serikali ilichunguza fedha zilizomo kwenye akaunti ya Escrow na ikabainika ni za Serikali suala lililoenda kinyume na mkataba uliokuwapo.

Kwa kutumia kipengele kinachoruhusu kufungua shauri nje ya mahakama za nchini kilichomo kwenye mkataba wa Tanesco na IPTL, Standard Chartered ilifungua kesi ambayo hukumu yake imeipa ushindi huo unaoitaka Serikali kulipa fedha hizo.

Akitoa ufafanuzi kupitia kaunti yake ya Twitter, msemaji mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema msingi wa kesi ni deni la benki hiyo iliyorithi kutoka kwa wakopeshaji wa Malaysia dhidi ya IPTL na si Serikali wala Tanesco.