Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahindi yaliyozuiwa yaondoka na vigogo, RC Kilimanjaro acharuka

Mahindi yaliyozuiwa yaondoka na vigogo, RC Kilimanjaro acharuka

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefanya ziara ya kushtukiza katika mpaka wa Holili wilayani Rombo, na kukuta shehena ya mahindi yakiwa yamepakiwa kwenye magunia eneo la soko la Holili, kwa ajili ya kusafirishwa Kenya kwa njia za magendo.

Rombo. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefanya ziara ya kushtukiza katika mpaka wa Holili wilayani Rombo, na kukuta shehena ya mahindi yakiwa yamepakiwa kwenye magunia eneo la soko la Holili, kwa ajili ya kusafirishwa Kenya kwa njia za magendo.

Awali mkuu huyo wa mkoa alihakikishiwa kwamba eneo hilo halikuwa na mahindi baada ya kurudishwa nchini.

Kufuatia hali hiyo amemuagiza Kamanda wa polisi mkoani humo, Amon Kakwale kuwachukulia hatua za kinidhamu mkuu wa kituo cha polisi Holili na askari wengine wawili waliokuwa zamu kwa uzembe wa kuruhusu mahindi kupelekwa Kenya kinyume na taratibu.

Mahindi ya Tanzania yamekuwa yakizuiliwa kuingia nchini Kenya kwa zaidi ya siku 21 sasa, kwa madai kuwa yana sumu kuvu. Hata hivyo, baadaye wataalamu walipima mahindi hayo na kukuta ni salama.

Mghwira alifanya ziara hiyo ya kushtukiza usiku wa kuamkia jana na kushuhudia shehena ya mahindi yaliyokuwa katika soko la Holili, huku mahindi hayo yakiwa yanabebwa kwa pikipiki na kupelekwa nchini humo kwa njia za magendo.

“Baada ya kutoka Holili jana kukagua hali ilivyo katika mpaka wa Holili, tulifuatilia kwa karibu kujiridhisha hii biashara ya magendo ipo ama la, lakini mchana niliuliza kama kuna kitu kinaendelea hapa mpakani, wakaniambia hakuna kitu kinachoendelea baada ya mizigo yetu yote ya mahindi kurudi nchini,” alisema na kuongeza:

“Sikuridhika kiasi cha kutosha, nilirudi ofisini nikafanya shughuli zangu kama kawaida, lakini nikatuma watu wangu watangulie kule mpakani, walipofika waliniambia bodaboda zinafanya kazi za kupakia mahindi kama mchwa yaani haraka haraka kuanzia muda wa saa tatu asubuhi kupeleka Kenya kwa njia za magendo.

“Halafu badala ya askari waliokuwapo kudhibiti ile hali, wao ndio wanawaambia wale vijana wa bodaboda ondokeni. Sasa kama askari wetu ndio mnatugeuka na kushirikiana na watu ambao wanatuvunjia sheria na kupoteza mapato na kutuharibia biashara, kwa utaratibu huu naomba askari hawa wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuruhusu hali hii ambayo inatuharibia biashara.’’

Hata hivyo, juzi kamati ya usalama ya mkoa huo ilifika eneo hilo kushuhudia shughuli zinavyoendelea, huku Mghwira akinukuliwa akisema kuwa biashara ya magendo imeongezeka kwa kasi katika mpaka huo, baada ya shehena za mahindi kuzuiliwa kuingia nchini Kenya kwa madai kuwa yana sumu kuvu.


Wasemavyo bodaboda

Mwananchi lilizungumza na baadhi ya vijana wa bodaboda ambao huwa wanasafirisha mahindi hayo kupeleka nchi ya Kenya, na kueleza kuwa biashara hiyo ya magendo huwapatia kipato cha kuweza kumudu maisha yao ya kila siku na kwamba wamekuwa wakiifanya kwa muda mrefu.

Emmanuel Sauli, mkazi wa Holili na dereva wa bodaboda, alisema kuwa tangu Kenya ikatae kuchukua mahindi ya Tanzania, wamekuwa wakisafirisha mahindi hayo kwa njia za magendo na kwamba biashara hiyo kwao ni ya muda mrefu.

“Sisi huwa tunachukua haya mahindi usiku wa manane na kuyapakia na kuyapeleka Taveta, ambapo tukifika tunakabidhi mizigo na wao wanapakia kwenye magari yao,” alisema Sauli.