Mahojiano na Diana Naivasha, Makamu Rais wa Bodi ya Shule ya Kifaransa, Dar es Salaam

Wednesday July 14 2021
mahojianopic

Diana Naivasha, Makamu Rais wa Bodi ya Shule ya Kifaransa, Dar es Salaam akiwa na mtoto wake wa miaka 10, Nnalekane ambaye anasoma katika shule hiyo.

S: Familia yako ni ya Kitanzania lakini mtoto wako ameandikishwa katika shule ya Kifaransa. Nini kimekufanya uchague shule hii?

D.N: Kaya yangu ni ya watu wasiozungumza lugha ya Kifaransa na inaishi kama Watanzania wen-gine tu. Nimekulia katika mazingira ambayo Kiingereza ni lugha ya pili au ya tatu. Nawashukuru wazazi wangu kwa kuhakikisha wana-nipatia elimu bora hususan waliponipeleka katika shule ya mkondo wa kati inayofuata mtaala wa Uingereza (English Medium) ambayo imeniwezesha kufahamu mambo mengi yaayoendelea ulimwenguni, kukutana na watu wa aina mbalimbali na kupiga hatua katika maisha.

Naamini kuwa lugha ya Kifaransa, ambayo kwa sasa ni miongoni mwa lugha zinazozungumzwa na watu wengi duniani, inakuwa muhimu zaidi katika dunia hii ambayo inaendelea kukubali mab-adiliko kila uchwao.

Hivyo, kama ambavyo wazazi wangu walivyonikuza katika elimu, ninataka kuhakikisha watoto wangu nao pia watanue upeo na uelewa mpana wa dunia kupitia lugha hii.

mahojianopiccc

 S: Ipi inaweza kuwa tofauti kubwa baina ya shule za Kifaransa na zile zingine za kimataifa zilizopo Dar es Salaam?

Advertisement

D.N: Nadhani wazazi wengi wanaweza kueleza ugumu wa kutafuta shule nzuri kwa ajili ya watoto wao. Hivyo, niseme, licha ya kuwa-po kwa chaguo kadhaa ya shule za ndani na kimataifa, lakini sisi tulikuwa na bahati ya kipekee ya kupa-ta shule ya Kifaransa yenye jumuiya ya wazazi ndani yake.

Hakuna shule nyingine ambayo inaweza kumpika vyema mwanangu katika umahiri wa lugha mbili (yaani Kiingereza na Kifaransa) kwa Dar es Salaam nikizingatia kuwa weledi wa lugha kwa sasa ni kitu cha lazima, hivyo shule ya Kifaransa ilikuwa ni chaguo sahihi zaidi kwetu.

Kwa kuongezea, shule hii iko chini ya Ubalozi wa Ufaransa na Wizara ya Elimu ya Ufaransa na ni sehemu ya Mtandao mkubwa wa Kimataifa wa Shule (AEFE) huku ikiwa na cheti cha ithibati kutoka kwa “International Baccalaureate and Cambridge English accredita-tion” na inaifanya shule hiyo kuwa ya gharama nafuu kuliko shule zingine za kimataifa.

S: Je, shule hiyo ya Kifaransa inakubali mtoto kutoka taifa lolote?

D.N: Ndiyo! Walimu wa hapa wengi wanafahamu na wanakumbatia misingi ya shule ya kutambua wanafunzi kutoka katika nchi yoyote na hapa si wanafunzi wote waliopo shuleni ni wazawa wa Ufaransa. Kiuhalisia, moja ya tatu ya wanafunzi wa hapa ni Watanzania. Walimu wa hapa wanahakiki-sha kuwa akili za watoto zinajengwa kupitia maarifa wanayotoa darasani huku wazazi nao wakionyesha ushirikiano wa karibu kwa kufuatilia na kuwaongoza watoto wao katika safari zao za kitaaluma.

S: Mwaka jana wakati wa maso-mo, kutokana na janga la Uviko 19, shule nyingi zilifungwa kwa wiki kadhaa. Shule hii ilikabiliana vipi na hali hiyo?

D.N: Janga hili lilisababisha biashara na shule nyingi kufung-wa na kutakiwa kufuata taratibu zilizokuwapo. Kilikuwa kipindi cha ‘kupimwa’ shule yetu kama inaweza kustahimili hali hiyo, na kuan-zia Machi mpaka Mei 2020, kipindi ambacho shule zilikuwa zikitakiwa kufungwa, pia na sisi tulihamishia madarasa yetu mtandaoni, kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa, kila siku.

Wakati wa wimbi la pili la Uviko 19, tukishirikiana kwa karibu na Ubalozi wa Ufaransa, shule hii iliweza kutekeleza miongozo ya kiafya iliyosaidia shule hii kuendelea na masomo, huku kukishuhudiwa shule zingine zikifungwa.

Uwezo wa shule hii kutokusitisha masomo kwa kipindi hicho ni uthibitisho wa dhahiri wa hatua zilizowekwa na uongozi, wazazi, wanafunzi na walimu za kukabiliana na majanga.

Mwanafunzi anapofika darasala 12, anaweza kusoma nini kwa masomo ya ngazi za juu?

D.N: Wanafunzi wa sekondari hupata fursa ya kushiriki katika program za mafunzo tarajali ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya kwenda katika vyuo vya kimataifa vya elimu ya juu.

Hadi anapohitimu darasa la 12, huyu anakuwa tayari ameshaandaliwa vyema kiakili na kitaaluma kudahiliwa katika vyuo vya nje ya nchi. Ufaransa ndiyo nchi ya nne duniani kwa kupokea wanafunzi wa kimataifa baada ya Marekani, Uingereza na Australia na pia ndiyo nchi ya kwanza kupokea wanafunzi wa kigeni wasiozungumza lugha ya Kiingereza.

Ni Ufaransa pekee ndiyo hutoa program za shahada ya uzamili 1265 zinazofundishwa kwa lugha ya Kiingereza na rahisi kufundishika. Mwaka 2020 takriban wanafunzi wa kimataifa 358,000 walichagua kusoma Ufaransa na idadi hii ina-ongezeka kila siku.

Tunahakikisha mpaka mahafali, wanafunzi hawa wanakuwa mahili wa lugha kadhaa, kuanzia ile lugha mama, Kifaransa, Kiingereza na Kihispania. Dunia ita-kuwa eneo lao la kujidai.”

S: Je, unawezaje kuielezea shule ya Kifaransa kwa neno moja? “Shule hii ya Kifaransa ni eneo sahihi kwa maendeleo ya dunia.

Advertisement