Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa awaongoza waombolezaji kumuaga Magufuli Mwanza

Majaliwa awaongoza waombolezaji kumuaga Magufuli Mwanza

Muktasari:

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumatano Machi 24, 2021  anawaongoza wakazi wa Mwanza na mikoa jirani kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli.

Mwanza. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumatano Machi 24, 2021  anawaongoza wakazi wa Mwanza na mikoa jirani kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli.

Utoaji wa heshima za mwisho unafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba uliofurika watu huku wengine wakifuatilia shughuli hiyo kupitia luninga nje ya uwanja.

Waombolezaji walioanza kuingia uwanjani hapo tangu saa 10 alfajiri huku baadhi wakiujaza uwanja wa ndege kuulaki msafara wa mwili wa Hayati Magufuli uliotokea visiwa vya Zanzibar.

Magufuli kupitishwa daraja la JPM Kigongo-Busisi

Pamoja na mawaziri na naibu mawaziri, hafla ya kutoa heshima za mwisho kwa Dk Magufuli anayetarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Chato Machi 26, 2021  pia imehudhuriwa na wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiongozwa na mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo.

Baada ya shughuli ya uwanjani, jeneza lenye mwili wa Hayati Magufuli litazungushwa kwenye mitaa mbalimbali jijini Mwanza kabla ya safari ya kuelekea Geita kupitia Kigongo-Busisi.