Makamba ateua wajumbe bodi ya Tanesco

Makamba ateua wajumbe bodi ya Tanesco

Muktasari:

  • Waziri wa Nishati, January Makamba amewateua wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).


Dar es Salaam. Waziri wa Nishati, January Makamba amewateua wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Taarifa kwa umma ya leo Jumamosi Septemba 25, 2021 iliyotolewa na Waziri imewataja wajumbe hao niĀ  Nehemia Mchechu, Zawadia Nanyaro, Lawrence Mafuru, Eng Cosmas Masawe, Abubakar Bakhresa, Eng. Abdallah Hashim, Balozi Mwanaidi Maajar, Christopher Gachuma.

Uteuzi huo umeanza leo Septemba 25.