Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makatibu Sadc waanza kupitia ajenda 13

Washiriki wa mkutano wa 39 wa makatibu wanaoshughulikia sekta ya afya na ukimwi Jumuiya ya maendeleo ya nchi kusini mwa Afrika (Sadc) wakifuatilia mkutano huo kwenye ukumbi wa BOT leo.

Muktasari:

Makatibu wakuu kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc) wa sekta ya afya na Ukimwi wameanza kupitia ajenda 13 za mkutano huo baada ya ufunguzi uliofanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Zainab Chaula.

Dar es Salaam. Mkutano wa makatibu wakuu wanaoshughulikia sekta ya afya na Ukimwi katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc) wameanza mkutano kwa kupitia ajenda 13 za mkutano huo.

Kuanza mkutano huo ni utangulizi wa mkutano wa mawaziri unaotarajiwa kufanyika Novemba 7 hadi 8 mwaka huu ambao utafikia makubaliano  yaliyojadiliwa na makatibu pamoja na wakuu wa taasisi.

Akifungua mkutano huo leo Jumatatu Novemba 4, 2019 Katibu Mkuu wizara ya Afya, Dk Zainab Chaula amesema Novemba 4 hadi 6 watajadili ajenda 13 ambazo kimsingi na kiutaratibu zinakuwa zimepitiwa katika ngazi mbalimbali za wataalamu.

“Baada ya majadiliano hayo tutajua sasa tunakwenda vipi kwa maana tutakuwa tumeshazipitia na tutakuwa tumeshakubaliana wote kwamba hizi ndizo ajenda za kutembea nazo na kuanza utekelezaji wake katika sekta ya afya na Ukimwi,” amesema Dk Chaula.

Aidha amesema asilimia 95 ya makatibu wakuu kutoka nchi 16 wanachama wameshiriki mkutano huo huku mawaziri 15 wakithibitisha kushiriki isipokuwa nchi moja.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu wa Sekretariet ya Sadc, Dk Willy Amis amesema asilimia 90 ya washiriki wa mkutano huo wameshiriki na kuthibitisha kuwepo, “Tangu Tanzania imepokea kijiti Julai mwaka huu, ushiriki wa mikutano ya Sadc umekuwa mkubwa na tunatarajia kutakua na mabadiliko makubwa pia katika utekelezaji wa ajenda zilizopo.”