Makonda: Diamond ruksa kukata viuno, wengine nitawatia ndani

Muktasari:

Apiga marufuku wasanii ambao hawajafanya jambo kwa jamii kusherekea na kujirekodi wakikata viuno kisha kuziweka mitandaoni.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam,  Paul Makonda amesema amempa ridhaa ya kutokuoa msanii Diamond na kumtaka aendelee kuwa ‘sukari ya mioyo ya watu’ sambamba na kuweka video za kukata mauno mtandaoni kutokana na alichokifanya kwa wakazi wa Tandale.

Makonda ambaye ni mlezi wa Kampuni ya WCB inayomilikiwa na Diamond amesema kwa kazi anayofanya huenda akioa mapema itamletea shida na kwamba anahitaji muda zaidi wa kufikiria kuwasaidia Watanzania wenzake.

Amesema, “Haya mambo mkiyajua vizuri bana kwanza ukiwa msanii halafu mashabiki wako wengi wakiwa wanawake ukioa wanaweza kukimbia, utafikiri ungewaoa wote,”

Makonda amewataka wasanii wote kuiga mfano wa Diamond wa kurudi na kusaidia jamii iliyowalea.

“Kwa alichokifanya Diamond hata nikiona video yake anakata mauno wala simfanyi, kitu Ila msanii hujafanya chochote halafu unasherehekea siku yako kwa kujirekodi video unakata mauno nakuweka ndani,” amesema.