Mambo matatu ya kipekee Mwenge wa Uhuru 2021

Muktasari:

  • Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amesema tofauti na miaka iliyotangulia, mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zilikuwa za kipekee kwa Watanzania.

  

Chato. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amesema tofauti na miaka iliyotangulia, mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zilikuwa za kipekee kwa Watanzania.

Akitoa taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru zinazofikia kilele leo Alhamisi Oktoba 14, 2021 mjini Chato, Waziri Mhagama ametaja maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru kuwa ni miongoni mwa mambo yanayofanya mbio za mwaka huu kuwa za kipekee kwa Watanzania.

Ametaja kitu kingine cha kipekee kuwa, mbio za mwaka huu zinafanyika wakati Taifa likiwa limewapoteza Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

"Tumekimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka huu huku Taifa likiwa limewapoteza viongozi wakuu wawili; Rais Magufuli na Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa," amesema Waziri Mhagama

Amesema Mwenge wa Uhuru umekimbizwa mwaka huu muda mfupi baada ya Taifa kupita kwenye  mabadiliko makubwa ya kiuongozi baada ya kifo cha ghafla cha Hayati Magufuli.

"Tunakushukuru na kukupongeza mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) kwa kutuvusha na kutuongoza salama," amesema Waziri Mhagama