Mamia ya waombolezaji wafurika mazishi mwanafunzi wa IFM aliyekatwa kichwa
Waombolezaji, ndugu na marafiki wakiendelea na ibada ya kuaga mwili wa James Temba.
Muktasari:
- Mwili wa James Temba (24) unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya familia yaliyopo katika Kijiji cha Mande, Kata ya Old Moshi Magharibi, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Moshi. Mamia ya waombolezaji wamefurika katika mazishi ya aliyekuwa mwanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM), James Temba (24), aliyeuawa kwa kukatwa shingo na mwili wake kukutwa ukiwa unaelea ndani ya maji katika Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam ukiwa hauna kichwa.
Temba, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha IFM, aliondoka nyumbani kwao Aprili 29, 2026 mwaka huu na baadaye mwili wake kukutwa katika mto huo, ukielea ndani ya maji, huku ukiwa umekatwa kichwa.
Waombolezaji, ndugu na marafiki wakiendelea na ibada ya kuaga mwili wa James Temba.
Mei 3 mwaka huu, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilithibitisha kifo cha Temba na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha kifo hicho, na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwili wa mwanafunzi huyo, utazikwa leo jioni katika makaburi ya familia yaliyopo katika Kijiji cha Mande, Kata ya Old Moshi Magharibi, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Hata hivyo, kwasasa shughuli ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo inaendelea nyumbani kwao na muda mfupi baadaye kutatolewa salamu za rambirambi kutoka katika makundi mbalimbali, ambapo baada ya salama hizo ibada ya mazishi itafuata.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.