Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manyara yatumia mabilioni ya fedha katika miradi ya maendeleo

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amesema katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Serikali imetumia mabilioni ya fedha katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, elimu, maji na barabara katika mkoa huo.

Babati. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amesema katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Serikali imetumia mabilioni ya fedha katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, elimu, maji na barabara katika mkoa huo.

Makongoro ameeleza hayo leo Machi 25, 2022 mjini Babati akitoa taarifa ya mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia.

Amesema sekta ya elimu ilipokea Sh21.4 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni ambapo madarasa 471 pamoja na bweni moja la wanafunzi wenye uhitaji maalum yamekamilika.

Amesema katika sekta ya afya walipokea Sh8.7 bilioni ambazo zimetumika kujenga vituo vya afya 23, zahanati 11, majengo ya dharura matano na kukamilisha ujenzi wa hospitali za wilaya.

Katika sekta ya maji amesema Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) walipewa Sh10.5 bilioni, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Babati (Bawasa) walipewa Sh8 bilioni ambapo wametekeleza miradi tisa na miradi 30 ipo kwenye hatua kadhaa.

Amesema sekta ya miundombinu kwa upande wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) walipewa Sh20.9 bilioni ambazo zimesaidia kujenga kilometa 792, ujenzi wa madaraja manne pamoja na kuweka taa za barabarani 219 katika mji wa Babati.

"Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (Tarura) walipokea Sh19.3 bilioni ambazo zimesaidia kufanya matengenezo ya barabara wanazozihudumia," amesema Makongoro.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bawasa, Honorath Sebastian ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za miradi ya maji na kuiamini Bawasa na kuwapa nafasi ya kusimamia miradi mikubwa kama mradi wa Orkesumet uliogharimu Sh41.5 bilioni.