Matokeo kidato cha nne haya hapa

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne 2021.

Matokeo hayo yametangazwa na Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Charles Msonde leo Jumamosi Januari 15, 2022.

Pia Baraza hill limetangaza matokeo ya upimaji wa Kitaifa wa darasa la nne, Kidato cha Pili 2021.

Dk Msonde amewataja wanafunzi 10 bora kitaifa kuwa ni pamoja na; Consolata Lubuva, Buthoi Nkangaza, Wilihelmina Mujarifu, Glory Mbele na Mary Ngoso, wote kutoka shule ya St. Francis Girls iliyopo mkoani Mbeya.

Wengine ni Holly Lyimo (Bright Future Girls), Blandina Chiwawa (St. Francis Girls), Imam Mogaeka (Feza Boys), Mfaume Madili (Ilboru) na Clara Assenga (St. Francis Girls).

Amezitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni; Kemebos (Kagera), St. Francis Girls (Mbeya), Waja Boys (Geita), Bright Future Girls (Dar es Salaam) na Bethel Sabs Girls (Iringa).

Shule zingine Maua Seminary (Kilimanjaro), Feza Boys (Dar), Previous Blood (Pwani), Feza Girls (Dar) na Mzumbe (Morogoro).